KAULI KUTOKA JUU ZAENDELEA KUWEKA PABAYA JESHI LA POLISI NA KUONEKANA TOFAUTI KWA WANANCHI.

Jeshi la Polisi bado linamhitaji Dereva wa Tundu Lissu ili kukamilisha upelelezi. Kwa sababu haiwezekani aendelee kupiga picha na kung’aa vile lakini wanasema ameathirika kisaikolojia". IGP Simon Sirro akiwa Mtwara.
NB:Ni sheria gani anaitumia IGP kuhoji uhalali wa Dereva wa Lissu kupiga au kupigwa picha, kuoga ama kufua nguo zake?
Kwani ni nani aliyemwambia IGP kwamba watu walioathirika kisaikoloji hawapigi au hawapigwi picha? Ni nani alimwambia kwamba walioathirika kisaikolojia hawaogi au hawafui nguo zao?
Kwani IGP anao ushahidi gani wa kitabibu unaodhibitisha kwamba muathirika wa kisaikolojia akipiga picha na kuonekana anang'aa huwa amepona tatizo la kisaikolojia?


Maoni ya watanzania tofauti juu ya maelezo yake hapo jana.


Maoni