MAGUFULI ANAENDELA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI BAADA YA KUMTEUWA KATIBU WA BUNGE NA Z KABWE.



Nimeyaona madai ya Zitto kuhusu Rais kumteua katibu wa bunge, Zitto anasema Rais kavunja sheria,wapo wanaosema Zitto ndiye kakosea na wengine wanasema Zitto yupo sawa.

Ukiisoma katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 87 peke yake bila kwenda kwenye sheria iliyofafanua kuhusu namna Uteuzi wa Katibu unavyotakiwa fanyika utaona Rais yupo sawa kwa asilimia 100!.

Lakini ukiisoma sheria ya utawala ya bunge ya mwaka 2016, iliyosainiwa mwezi Machi mwaka jana (2016), kifungu cha 7(3) kinaeleza kuwa Katibu wa Bunge atateuliwa na Rais kutoka kwenye majina matatu yaliyopendekezwa na kamati ya bunge.

Sheria imetumia neno "shall" na siyo "may" kwa maana imemtaka Rais kutokwenda kinyume na matakwa hayo.

Kama sheria ingetumia neno, "The president may" kusingekuwa na huu mjadala, lakini ukikisoma hicho kifungu, kimemfunga Rais kwa kutumia neno "Shall" neno hili kwa watu wa sheria linapotumika maana yake huna njia nyingine zaidi ya ilivyosema sheria.

Ufafanuzi wa Tume hiyo umetajwa kwenye kifungu cha 12 cha sheria hiyo, kimetaja wajumbe wote wanaoinda Tume hiyo ya Bunge.

Yawezekana Zitto kawauliza wajumbe wa Tume inayoundwa chini ya sheria hiyo ama labda nae ni mjumbe kama walipendekeza majina na kupata taarifa za Tume kutopendekeza majina ndiyo maana Zitto kasema hayo. Kihabari, Zitto ni chanzo sahihi kisichotiliwa shaka kuhusu masuala ya Bunge.

Kinachotakiwa ni kupata ukweli kutoka kwa chanzo mamlaka ambacho ni Spika wa Bunge aliyetajwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo athibitishe madai hayo ya Zitto.

Kifupi ni kwamba, kwa mujibu wa sheria Rais hatakiwi kuteua tu Katibu wa Bunge, atateua kutoka kwenye orodha ya majina matatu yaliyoletwa kwake na Tume.

Ili kujua kama Tume ya Bunge ilipendekeza majina ama lah, kazi ya wanahabari sasa kuendeleza "story" hii kwa kuwauliza wajumbe wa tume hii kama walitakiwa kupendekeza majina ama lah.

Naamini "a day two journalism" itakuja na jibu la mjadala huu! Ijapokuwa story hii inaweza athiriwa na dhana ya usiri wa taarifa za serikali, lakini imetoa fursa nyingine ya habari ya uchunguzi kama kweli Rais kavunja sheria ama Zitto hakuwa na taarifa sahihi.

Ila wanasheria wana taratibu zao, pale Sheria na Katiba zinapogongana, ipi huzingatiwa? Wanasema ni Katiba ndiyo humaliza mvutano huo wa kisheria.

Lakini kama ndiyo hivyo na kama kweli Rais kateua bila kufuata sheria ya utawala ya bunge? Swali ni je, kwanini kafanya hivyo? Haiamini Tume ya Bunge? Ama kuna ajenda ya kuibua mjadala mpya na kuzima mengine yanayotawala kwenye mijadala ya kitaifa kwa sasa?

Naamini media itakuja na majibu ya ukakasi huu, kama siyo Jumatatu basi Jumanne! Hapa kuna sources nyingi kweli kweli, Spika anaweza kuwa bias kutokana na muingiliano wa kimhimili, wajumbe nao ni vyanzo muhimu sana hapa, wajuzi wa sheria nao ni muhimu pia ili watupe tafsiri ya kisheria kuhusu inavyo tamka sheria na inavyotamka katiba!.

Maoni