MIAKA MIWILI WATANZANIA WANAENDELEA KUSUBILI EMBE CHINI YA MFENESI



MIAKA MIWILI WATANZANIA WANAENDELEA KUSUBILI EMBE CHINI YA MFENESI 
Leo tarehe 25-10-2017, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakamilisha miaka(2) ya uongozi wa serikali mpya ya awamu ya tano, chini ya Rais John Joseph Pombe Magufuli na makamu wa Rais Bi. Samia Hassan Suluhu. Tunakila sababu ya kufanya tathimini(evaluation) ya mafanikio tuliyopata na changamoto ambazo bado zinaendelea kutukabili kwa kipindi cha hii miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano.
CHANGAMOTO:
1. AJIRA, suala la ajira limeendelea kuwa changamoto katika serikali ya awamu ya tano kuna wahitimu (graduates) wa vyuo vikuu tangu mwaka 2015, 2016 na 2017 wakiwemo walimu, madaktari, wauguzi, maenginia, wahasibu, wanasheria na fani mbalimbali ambao bado hawajapata ajira 

2. UMEME, suala la umeme bado ni changamoto, licha ya umuhimu mkubwa wa nishati ya umeme lakini baadhi ya maeneo ya mjini na vijijini umeme bado ni changamoto (leo saa 06:30 umekata tanzania nzima)
3. MAJI, suala la maji bado ni changamoyo kwenye maeneo mengi ya tanzania yakiwemo ya mjini na vijijini, licha ya maji kuwa ni muhimu kwa uhai wa mwanadamu lakini tanzania tatizo la maji bado ni kubwa na linatesa watanzania wengi
4. KILIMO, suala la kilimo bado ni changamoto, licha ya kusema Kilimo ni uti wa mgongo wa tanzania, lakini sekta ya kilimo bado imekuwa na matatizo mbalimbali yakiwemo: uhaba wa pembejeo na dawa za kisasa kwa wakulima wadogodogo, teknologia duni kwa wakulima wadogodogo, uhaba wa masoko na bei duni ya mazao ya wakulima
5. MIKOPO YA ELIMU YA JUU, suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu bado ni changamoto kwenye taifa letu, licha ya ghalama za kuomba mikopo kupanda mwaka hadi mwaka lakini upatikanaji wa mikopo hasa kwa vijana masikini bado imekuwa ni kitendawili
6. USAFIRI, suala la usafiri bado ni changamoto licha ya juhudi za serikali kununua ndege aina za Bombadia na kufufua shirika la ATCL lakini changamoto bado ni kubwa kwa wasafiri wa usafiri wa nchi kavu, foreni nazo bado ni kitendawili hasa katika mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya mikoa mingine,
7. MISHAHARA NA MADARAJA KWA WATUMISHI WA UMMA, suala la kupandishwa madaraja na mishahara bado ni changamoto, watumishi wa umma wanaishi kwa mikopo na kuungaunga kwani mishahara yao ipo palepale licha ya gharama za maisha kupanda, sheria ya utumishi inaruhusu kila mtumishi kupata haki ya kupanda daraja na mshahara kitu ambacho kwa miaka miwili sasa kimekuwa cha kusuasua kwa sababu ya zoezi la vyeti feki na ukaguzi wa kugushi umri
8. BIASHARA, suala la biashara ni changamoto, licha ya umuhimu wa sekta hii kwenye ukusanyaji wa kodi lakini mazingira ya kufanya biashara kwa tanzania yamekuwa ni magumu sana, kila mfanyabiashara analalamika si mkubwa wala mfanya biashara ndogondogo wote wanalia na kusema hakuna biashara,
9. AFYA, suala la afya bado ni changamoto kwa taifa letu, kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya watoto wadogo chini ya miaka 5, kumekuwa na ongezeko kubwa la AFYA YA AKILI ripoti ya hivi karibuni inaonesha ongezeko kubwa la afya ya akili katika nchi ya tanzania, madawa, madaktari, wauguzi, vitanda na vifaa vya hoapitali bado ni changamoto pia
10. WATU WASIOJULIKANA, siku za hivi karibudi kumekuwa na matukio ya uharifu kuongezeka, watu kuuwawa, watu kutekwa, watu kupigwa risasi, watu kuteswa na watu wasiojulikana. Watu wasiojulikana wamekuwa ni changamoto sana kwa taifa letu, watu wasiojulikana walimteka Ben Rabiu-Saanane, Roma Mkatoliki, Mon n.k, watu wasiojulikana walimpiga Tindu Lissu risasi zaidi ya 38 mchana kweupe, watu wasiojulikana wameua ndugu zetu wa KIBITI, watu wasiojulikana wameua Askari Polisi ukonga, hawa watu wasiojulikana wamekuwa ni tishio kwa taifa, hii pia ni changamoto kubwa katika serikali ya awamu ya tano
MAFANIKIO:
1. Tumefanikiwa kununua ndege na kufufua shirika letu la ATCL, licha ya shirika hilo kuendelea kuwa na changamoto ya marubani na wafanyakazi ili kuleta ushindani katika soko la usafiri wa anga, elimu pia lazima itolewe ili wananchi wa kawaida wafahau juu ya ndege zao hasa katika maeneo ya vijijini, mtakumbuka Mhe. Nappe aliulizwa maana ya Bombadia na wapiga kura wake kule mtama.

NINI KIFANYIKE:
1. Tuendelee kusubili embe chini ya mfenesi

2. Tukasome ILANI ya chama cha mapinduzi, ili tujui yalioandikwa yanaweza kukamilika ndani ya miaka mitatu iliyobaki(hii ilani inapatikana mtandaoni bure au nenda ofisi ya chama cha mapinduzi watakupa)
3. Tuendelee kuwa wavumilivu nchi ipo kwenye mabadiliko(transformation)
4. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

  Maoni Ya Willy C Tarimo

Maoni