ZITTO KABWE AACHIWA NA KUKAMATWA TENA SABABU KUBWA HII HAPA.


Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, aachiwa na kukamatwa tena kwa maelekezo ya ofisi ya afisa upelelezi wa makosa ya jinai
Mbunge huyo wa Kigoma mjini, alikamatwa mara ya kwanza asubuhi ya Jumanne nyumbani kwake mjini Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi Chang’ombe.
Baada ya saa kadhaa mbunge huyo aliachiliwa huru kabla ya kukamatwa tena.

Wakili wake Stephan Ally Mwakibolwa anasema sababu zilizotajwa kwa kushikwa kwake ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.

Kauli kubwa haswa wanayosema ni kuihusisha serikali ya CCM na matukio ya watu waliookotwa katika fukwe za bahari ya hindi wakiwa wamefariki ,pamoja na tukio la mbunge Tundu Lissu” amesema Mwakibolwa.

Maoni