MUNGU AKISIMAMIA KITU AMNA AMBAYE ANAWEZA KUPINGA,,MBOWE ASEMA AFYA YA LISU YASIMAMA VYEMA.



Ndgu waandishi wa habari tukio la Lissu sio la kusita kusema Serikali inahusika kwa asilimia zote!!,,mpaka sasa katika uchunguzi wetu tumebaini CCTV kamera zishaondolewa lile eneo ambalo Mh Lissu alidhuriwa!! Je ni kwa nini imeondolewa!! Hapa bila kumung'unya Maneno serikali inahusika kabisa!!
Tunaposema tunahitaji vyombo vya nje vya kiuchunguzi hatumaanishi kuwa vyombo vya ndani havina uwezo,,,,,Bali vyombo vya ndani havina Dhamira kuhusu hili tukio!!
AFYA YA LISSU!!
Afya ya Mh Lissu imeendelea kuimarika sana tena sana!! Wiki iliyopita Ndiyo ametoka ICU ,,Mashine zilizokuwa zimewekwa ili kusukuma mwili wake,kwa ajiri ya kuvutia hewa ya oxygen,kula, kwa sasa zimeondolewa zote na anaweza kula mwenyewe,kupumua mwenyewe,kutembea mwenyewe!! ,,,,Juzi ametembea mwenyewe ,,na alitembezwa kwenye wheel chair na akaliona jua kwa Mara ya kwanza akiwa Kwenye wheel chair Nairobi tangu ashambuliwe!!
Baada ya wiki moja Lissu atamaliza sasa awamu ya Pili ya matibabu yake na ataenda tena awamu ya tatu,ambapo itakuwa nje ya Nairobi ,,,,na nje ya Tanzania ,,,kwa sababu za kiusalama sitazungumzia hilo leo!
MICHANGO KWA LISSU!!
Suala la michango kwa Mh Lissu limeendelea kwa moyo wote kabisa na kwa kila mtanzania yeyote bila kujali itikadi ya chama wameendelea kumchangia!! Mpaka sasa michango ni kama ifuatavyo!!👇🏼👇🏼
Wabunge wa CHADEMA 48,465,000 Tsh mil
Kundi la watanzania wote = 24,200,000Tsh mil
CRDB =90,857,217 Tsh Mil.
Wabunge wote kabisa = 43,000,000Tsh Mil.
Diaspora {Wanachama walioko nje ya Tanzania} = 29,700 us Dollar.
Wafanya biashara wadogo wadogo na wa kati =18,000$ =40,500,000 Tsh mil.
GHARAMA ZA MATIBABU.
Mpaka tar 12/10/2017
Septemba,,,10,687,316Ksh = 106,873$ =240,464,250 Tsh mil.
October,,,,,,10,378,158 us Dollar.
Gharama ya Madktari ni Ksh 4,644,000 ambalo ni jopo la madaktari 12 wanamhudumia!!
Madaktari,Thieta,Damu na kila kitu cha msingi ni = ksh 18,352,156= 412,472,250 Tsh Mil.
Bado safari inaendelea,,Tumaini letu Lissu atarudi barabarani na ataendelea kuwatetea watanzania na watafaidi uwepo wake!!
Awamu ya tatu sasa kwa saababu Mh Lissu yuko stable kiafya sisi kama chama tutawaachia sasa wanafamilia waweze kuteta na Mh Lissu na sisi tutakuwa nyuma kuisapoti familia,,,lakini nitahadharishe hatutaiacha familia kwa kila kitu!! Lissu ni Bora kuliko Pesa!!

Mbowe amewaambia wanahabari kwamba kwa mujibu wa madaktari, hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu imeimarika hivyo wakati wowote kuanzia wiki ijayo anaweza kutolewa hospitali.
"Bw Lissu ametolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwekwa katika wodi ya kawaida huku akiwa na uwezo kamili wa kuongea na kutembea kwa kutumia kiti cha magurudumu," alifafanua Mbowe. Hata hivyo, Chadema imesema kuwa, kwa kuhofia usalama wa Lissu, kwa sasa hawatamrudisha nchini Tanzania.
"'Kwa sababu za kiusalama hatutaweza kusema atakwenda wapi lakini itoshe tu kuwaambia kuwa ataanza awamu ya tatu ya matibabu nchi nyingine, sio Tanzania wala sio jirani''

Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya thelathini na watu ambao mpaka sasa hawafahamiki mwanzoni mwa mwezi jana huko mjini Dodoma alipokuwa akihudhuria vikao vya bunge. Hivi karibuni, ndugu zake Bw Lissu wameitaka serikali kuvishirikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa kama vinavyoshirikishwa katika mambo mengine ili kuongeza ufanisi katika upelelezi huo.
Jeshi la polisi nalo limeomba lipewe nafasi wa kufanya upelelezi.Tundu Lissu yuko nchini Kenya kwa takribani wiki nne sasa kwa ajili ya matibabu.

Maoni