MWANAHABARI MANSOUR ASEMA NJAA NA KUTOJIAMINI NDIVYO VINAYOWEZA MSUMBUA MURRO.


Nimechukua muda kumsikiliza kijana Jerry.C.Murro dhidi ya tuhuma, malalamiko na namna alivyotumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Mrisho Gambo kuja kumtangaza (kumbrand) juu ya Shughuli alizozifanya mkoa wa Arusha na kutumika pia kuonesha kuwa hakuna Jambo lolote alilolifanya Mbunge wao wa Arusha ,Mh Godbless Lema.
Pia nimechukua muda wangu kumsikiliza Jerry Murro akijigamba juu ya mambo aliyowahi kuyafanya katika taifa hili ikiwa ni pamoja na kupewa tuzo mbili za uandishi wa Habari za Uchunguzi, ni kazi nzuri Lakini Si kweli kuwa Jerry Murro ndie mwandishi pekee aliyejitwalia tuzo hizo.
Tuzo hizo hata sie tunazo tumezifungia makabatani na zinaliwa na michwa tu,tena hizo hizo za Uchunguzi,lakini kuna waandishi wengi nchi hii wamewahi kufanya habari za Uchunguzi zaidi yako na zaidi ya ulichokifanya wewe na baadhi yao nikutajie tu wachache ambao ni magwiji wa habari za uchunguzi nchi hii ni pamoja
Dotto Bulendu (Report ya Sumu mgodi wa North Mara,Kuna njaa Tanzania au hakuna,)nk. Mansour Jumanne (Mapigano vikundi vya Uhalifu na kigaidi Musoma)
Eagan Salla, Ansbert Ngurumo, Neville Meena, Fredrick Katulanda, Kibanda
Juma Mudimi, Martne Nyoni, Akina Malissa Chilumba, Waandishi wa Mwananchi juu ya issue ya Escrow na nyingine, Balile na Manyerere, hawa ni baadhi ya Waandishi wenye heshima kwenye nchi hii juu ya mambo ya uchunguzi. Kwa hiyo, watanzania msitishike sana kuwa Jerry Murro ndio gwiji sio kweli.
Nikisema leo kuwa Jerry C. Murro anatumika kama "SPONGER"nitakuwa sijakosea na kwa tafsiri ya Lugha ya kimombo inasema
"is one who habitually takes advantage of the generosity of others without making any useful return"
Hiki ndicho Wanaccm na Mkuu wa Mkoa arusha wanamfanya kijana Mwenzetu,baada ya Mtu kama Mrisho Gambo kupambna kwa kila njia kutengeneza Chuki na kujipendekeza kwa wanaArusha lakini wapi.Arusha haiitaji hasira
Kuna hoja tatu dhaifu ambazo Jerry C.Murro ameandikiwa na Mrisho Gambo pamoja na baadhi wapambe ambazo inawezekana zikawa hoja za kwanza dhaifu duniani kuwahi kutokea
1.KAZI ALIYOKUWA ANAFANYA LEMA KABLA YA KUWA MBUNGE,
Kila mtu nchi hii anataka kuwa na maisha mazuri na kila mmoja nchi hii kafight anavyojua ,katumia njia tofauti kutaka kufika anapopataka ni moja kati ya njia za mafanikio, kuna matajiri wakubwa saizi lakini historia inaonesha waliwahi kuwa majambazi, kuna Vingozi wa Jeshi la Polisi waliwahi kutuhumiwa kuwa wanatumiwa na wahalifu, hata juzi Mhe.Makonda kuna baadhi ya askari aliwataja kuhusika kuuza dawa za kulevya, lakini lengo lao nikufanikiwa kimaisha hata Mhe.Rais Magufuli kuupata Urais kuna mahala alitoka, na kuna mambo alifanya.
Jerry C. Murro wewe sio wa kwanza Nchi hii kutajwa katika issues tofauti, Wewe si Malaika kusema hauna Makosa ,Wewe si mtimilifu kama unavyodhani,na ni nani aliyemtimilifu labda unisaidie ?
Wewe leo tukianza kusight Maisha yako kuanzia utotoni hadi leo ,unadhani hauna mabaya yako?,hauna Ujinga wako ?au na wewe unataka tuseme? Hapana hatuwezi kusema kwa sababu inawezekana ulitubu na Mungu wetu wa Mbinguni alikusamehe.
Je sie wanadamu nini tuseme ? Kwahiyo issue ya kuwa Lema alikuwa sijui ni nani ata angekuwa Jambazi,Malaika ,as long as alijireview na kuamua kuacha iyo ni Credit kwa lema na tunatakiwa kumpa Mungu sifa na Utukufu tunaambiwa Jambazi mmoja akiokoka malaika Ushangilia ,
Kwani mbona Katika Chama chetu cha CCM kuna mafisadi,kuna watunga sheria wabovu ,waingia mikataba wa ovyo,Wahujumu uchumi wanatofauti gani na Majambazi hao?,wanatofauti gani na wauaji hao?wanatofauti gani na wachuna ngozi hao? Wanatofauti gani na wauaji hao? Tumshukuru Mungu kwa kila atambuaye makosa yake na kutubu .
2.KUNA WADADA CHADEMA WANASAGANA 
Jerry Murro siku zote Mchawi umjua mchawi mwenzie ,Msagaji umjua msagaji mwenzie ,Shoga umjua Shoga mwenzie ,sasa wewe umewajuaje hawa? Lakini suala mapenzi ni issue ambazo ziko too personal , leo tukisema mbna tuna baadhi ya mawaziri wanawake hatujui waume zao je wao ni wasagaji akiwepo mmoja mkubwa kabisa ? Na je ukiambiwa Uthibitishe utakuwa tayari kuonesha Usagaji uo wanafanyia wapi au nani umewahi kufanya naye Usagaji?
Alafu hizi sio hoja bali na hasira kaka ,punguza jazba kama ni issue ya Wabunge au wadada kutokuwa na Waume isikuume,
3.MRISHO GAMBO NDIO KAVAA VIATU VYA LEMA,
Rafiki yangu Murro maana ya kusema unatumiwa kama Toilet paper ni hii,Mrisho Gambo hawezi kuvaa viatu vya Lema hata Kanda mbili hawezi,alafu Jerry sijui hapo Tumaini Critical thinking hamkusoma? Sijui hapo tumaini ukufundishwa how to make a story? Sijui hujui Theories of Masscommunications zinavyofanya kazi maana umetumia Muda mrefu kuelezea Jimbo la Arusha na kazi anazofanya Gambo,
Mie nikufundishe siku zote Branding Campaigne haifanyi hivyo ulichokifanya wewe ni Staged News,na sio Branding njoo tukupe Shule ya namna ya kufanya Branding,
Nimesikitika saana kuona rafiki yangu Murro kutokujua hata majukumu ya Mbunge na Majukumu ya serikali yetu,ulichokifanya wewe Umeamua kumdhalilisha Mh Rais kuwa hapeleki maendeleo Arusha, na sio lema kama ulivyokusudia na elewa Murro anachokifanya Gambo ni sehemu ya majukumu yake haitaji hata kupigiwa kofi moja.
Nimalize tu nakusema JERRY.C.MURRO NA MRISHO GAMBO MAJIMBO YA ARUSHA HAYAITAJI HASIRA,
Tuendelee kupambana na hali zetu na tuendelee kumtia moyo Mh Rais kwenye utekelezaji wa Serikali ya Viwanda lakini kuwa toilet paper haitatusaidia katika maisha zaidi tunaua Credibility zetu na kuaibika mbele ya jamii zetu
Mansour Jumanne,
Mchunguzi

Maoni