NANI AMBAYE AWEZE KUAMINIKA KATI YA SERIKALI NA ACACIA MAANA WANANCHI WAPO NJIA PANDA.


Serikali ilikiri kupitia kurugunzi ya mawasiliano - ikulu chini ya Greyson Msigwa kuwa Acacia wamekubali kulipa kiasi fulani cha fedha, dola million 300,. Tena Rais akasisitiza "Naomba Barrick walipe hizo Tsh. Billion 700 haraka kwa sababu nina taka kuzitumia"

Sasa Leo Acacia katika press release yao wanasema hawana uwezo wa kulipa hiyo pesa na hayo makubaliano kwanza wanadai hawaja yaona.!

Kwa mazingira haya ni nani muongo? Au wameamua kutu-confuse baada ya kushindwa kutu- convince ?

Chanzo cha haya ni nini? Serikali imetoa wapi hayo makubaliano ya kulipana?

Au walio tumwa kuiwakilisha Barrick hawaja peleka taarifa kwa wakubwa wao? Kuna maswali mengi na yasiyo na majibu! Labda sizonje (aliye nje aingie ndani)

Narudia kusema, kabla ya kuingia katika vita yoyote hakikisha jambo moja muhimu , 'unajua ubora na udhaifu wa adui yako' , Vinginevyo utakuwa umechagua kushindwa kabla vita yenyewe kuanza!

Mabepari hawana 'win to win situation' ! Eti unaketi meza moja na bepari utegemee glory game!? Ni rahisi kwa Taifa stars kushinda na kuchukua kombe la dunia mwakani, ila si usawa katika biashara na mabepari!

Naiona hatari kubwa sana inakuja, hawa watu wakienda mahakamani, pia tusitegemee haki kulalia kwetu, labda kama kesi itafanyika katika mahakama ya Kisutu!

Mwisho, Sheria zilizopo si kwa faida ya wananchi, bali zilitungwa kulinda utawala na tabaka Lao.


Maoni