NUKUU ZA MWALIMU NYERERE AMBAZO ZINAENDELEA KUBAKI KATIKA KUMBUKUMBU YA WATANZANIA.


NYERERE DAY: 
Top 10 ya nukuu za Mwalimu Nyerere
#10.Amani ni zao la matumaini,pindi matumaini yanapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
#9.Mnaingia karne ya ishrini na moja mmepanda basi la ukabila,mnaona sifa kuulizana makabila..mnataka kutambika?
#8.Ukimwona mtu anakwambia jambo la kipumbavu na yeye mwenyewe anajua kuwa unajua ni lakipumbavu ukakubali ujue amekudharau.
#7.Ni bora kuishi na fikra hai kuliko kuishi na fikra zilizokufa
#6.Unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda fulani na baadhi ya watu wakati wote,ila huwezi kudanganya watu wote kwa wakati wote.
#5.Inawezekana tatizo la Paka kwa Panya lingekwisha kama paka angefungwa kengele shingoni.Tabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo.
#4.Tusiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu
#3.Ikithibitishwa mahakamani kuwa mtu ametoa au kupokea rushwa hatukumwachia hakimu pekeyake,.Tukasema atakwenda ndani kwa miaka miwili na viboko 24,,kumi na mbili siku anaingia,kumi na mbili siku ya kutoka akamuonyeshe na mkewe
#2.Hakuna umasikini mbaya sana kama umasikini wa mawazo.Ni mbaya sana
#1.Njia pekee ya kumsaidia masikini ni kumsomesha mtoto wake.
By •Mwlm Nyerere

Maoni