SAKATA LA VYETI SASA LAWAKUMBA WABEBA MISTIMU NA WACHIMBA MASHIMO TANESCO NAO WATAKIWA KUWA NA VYETI.

Baada ya sakata la vyeti feki kupamba moto serikali sasa limeweza kutinga katika mashirika yote ya umma baada ya waraka kusambazwa katika mashirika yote ya umma mtu ambaye atakuwa ana vyeti vya form four basi ndio mwisho wake,

Uws Media imeweza kukutana na wafanyakazi wa tanesco ambao walikuwa ni vibalua wa kubeba nguzo pamoja na kuchimba mashimo ya kueleza kuwa wanatoka katika nafasi zao kutokana na kushindwa kuwa na vyeti vya form four na sasa wanasubiri posho zao ili waweze kutoka,

Uongozi umeweza kutoa taarifa kuwa mpaka kufikia kwezi wa kumi wafanyakazi wote waweze kutoka na sasa kuhusu tanesco ni nchi nzima kuna watu awana kazi kutokana na vyeti,

Wafanyakazi wa kubeba nguzo na kuchimba wameweza kutoa lawama kubwa kwa serikali kwanini wanafanya hayo kwani kazi ya kubeba nguzo na kuchima mashimo ni nguvu ya mtu na sio kuwa na vyeti,
Kuna mashirika ya umma mengi hapa nchini ambayo yanaendelea kufukuza watu kuhusu vyeti ila tutaendelea kuwaletea habari hizi za kufukuzwa kwa watumishi wa mashirika ya umma kuhusu sakata la vyeti feki.

Source Uws Media

Maoni