Muungano wa upinzani nchini Kenya
National Super Alliance (Nasa) umefutilia mbali maandamano ambayo
yalikuwa yamepangiwa kufanyika nchini humo leo kushinikiza mageuzi
katika tume ya uchaguzi.
Muungano huo, kupitia taarifa, umesema
umechukua hatua hiyo kupata fursa ya kuomboleza watu ambao wameuawa
kwenye maandamano ya awali.Nasa, muungano unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, ulikuwa umeahidi kufanya maandamano kila siku kushinikiza mageuzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.
Taarifa iliyotumwa na msemaji wa Bw Odinga, Dennis Onyango, imesema maandamano hayo yatarejelewa tena Jumatano.
Uchaguzi mkuu umepangiwa kufanyika tarehe 26 Oktoba baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti na kuagiza uchaguzi mpya wa urais ufanyike katika kipindi cha siku 60.
"Hii ni hatua ya muda ya kuuwezesha muungano huu kuwazuru na wafuasi wake waliokumbana na ukatili wa polisi na jamaa za waliojeruhiwa au kuuawa," taarifa hiyo ilisema.
Jumatatu, kijana wa miaka 18 aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani mjini Kisumu.
Waliouawa maandamano ya baada ya uchaguzi Kenya 33
Watu ambao Amnesty na HRW wanasema waliuawa na polisi Nairobi
-
67 Idadi ya watu ambao mashirika hayo mawili yanakadiria waliuawa kote nchini Kenya
-
9 Umri wa Stephanie Moraa Nyarangi aliyepigwa risasi Mathare
AFP/Getty
Mashirika mawili ya kutetea haki za kibinadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch jana yalisema watu 67 wameuawa tangu kuanza kwa maandamano ya upinzani baada ya uchaguzi.
SOURCE BBC
Maoni
Chapisha Maoni