WAKATOLIKI WAENDELEA KUMPINGA PENGO JUU YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NCHINI TANZANIA.



Napata shida sana kugusa au kuongelea jambo juu ya viongozi wa dini kwa maana imani yangu inanikataza kufanya hivyo.
Ila kunawakati inalazimika kumkosoa kama atakuwa anafanya Kama binadamu na kitu ambacho nikinyume na kondoo zake hapo lazima nao tuwakemee maana wao sio malaika
Nimesikitishwa sana na maneno aliyoyasema kiongozi wangu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni kardinali huyu ni Askofu Pengo wa Kanisa katoriki jimbo kuu la Dar
Jana kajitokeza kupinga maoni ya askofu mwenzie ambaye ndiye msemaji wa maaskofu wa RC na ndiye kiongozi wa baraza la maaskofu Tanzania Mhasham Baba askofu Severine Niwemugizi
Nanukuu alivyosema Askofu Pengo Alisema "swala la katiba mpya si agenda ya Kanisa katoriki na wala Kanisa halijiusishi na siasa aliyoyasema askofu Severine Niwemugizi ni yakwake" mwisho wa kunukuu
Baba askofu kardinali Pengo naheshimu sana nafasi yako na huduma yako ila hapa omepotea sana sana tena sana
Kwanza wewe sio msemaji wa Kanisa pili siasa na Kanisa ni kulwa na doto ni vitu pacha.Alicho kisema msemaji wa Kanisa katoli ambaye ndiye kiongozi wa maskofu wa Kanisa katoriki Tanzania hakukosea kwa idhini ya katiba yenu yeye ndiye anawasemea sasa huwezi mtofautisha na lolote atakalolisema
Inawezekana kanisa halijiusishi moja kwa moja na siasa ila kama watanzani/wananchi mnatakiwa kutoa maoni na ushauri juu ya hali ya kisiasa ilivyo hii kwa mujibu wa katiba yetu ambayo inawatambua nyinyi viongozi wa dini
Pili wakati wa bunge la katiba viongozi mbalimbali wa dini walichaguliwa wakiwepo maaskofu wa kanisa unalokiongoza tena nakumbuka mkatoa waraka wa baraza lamaaskofu sikuona ukipinga Leo katiba imetelekezwa, fedha za watanzania zilitumika anajitokeza jasiri na kukumbushia unaona nidhambi hili Baba askofu Pengo nakupinga kanisani na nje ya Kanisa bila woga
Uache woga na urafiki ulionao na serikali ukasahau kuna watanzania zaidi ya mamilioni wanasubiri katiba hiyo
Nategemea utarekebisha kauli yako kwa maslai mapana ya taifa hili la Mungu Tanzania
Mungu ibariki Tanzania 
Mazoko Allen

Maoni