WALIOPIGANIA CCM KUBAKI MADARAKANI LEO HII NDIO WANAONEKANA WABAYA NDANI YA CHAMA CHAO,,KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA.


Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015, baada ya watu wa CCM akina Nape na Kinana kugundua kuwa CCM haitakubalika wala haitaaminiwa tena na wananchi kwenye uchaguzi ule, waliamua kutumia mbinu ya kuwaaminisha wapigakura kuwa wanamchagua Magufuli na sio CCM.
Ili kuliweka sawa hilo na kuwachanganya watu ili wasahau kwamba huyo Magufuli hatokei ndani ya hiyo CCM iliyooza (sijui watu wadhani kuwa ni mgombea huru asiyetokana na chama) wakabuni mbinu ya kumhenyesha mzee wa watu kwa push-up majukwaani huku akieleza ahadi lukuki zilizowafanya watu wachanganyikiwe ndani ya muda mfupi wa mwezi mmoja wa zile kampeni.
Akaahidi mahakama ya mafisadi akisema akiingia Ikulu ataanza kuyafunga aliyoyaita "mafisadi papa" huku watu kwa asilimia zote wakaamini kuwa Edward Lowassa na wengine wote hasa wale wa kashfa za Lugumi na Escrow akina William Ngereja, Endrew Change na wenzao wote wangekuwa wa kwanza kuburuzwa kwenye mahakama hiyo ya mafisadi, kumbe ulikuwa ni mchezo wa danganya toto. Usiniulize ni wangapi waliofikishwa kwenye mahakama hiyo tangu ianzishwe maana sijasikia popote.
Akaahidi Millioni 50 kila Kijiji na kupambana na Rushwa, msiniulize kuhusu utekelezaji wa hayo ulipofikia maana binafsi sijaona chochote.
Leo hii baada ya hali ya nchi kubadilika na wananchi kuteseka, huku wengine wakijitahidi kupambana na hali zao bila mafanikio, sasa hivi kila kona ya nchi hii (sio watu wa CCM wala sio wapinzani) wote wanaitupia lawama CCM hadharani huku wakisahau kuwa walichanganyikiwa na push-up, wakaona mvinyo wa dodoma wakadhani ni mbege ya uchagani.
Ahahahahaah! mimi nacheka maana wote hivi sasa (sio wa upinzani wala sio wa CCM) wote tunapambana na hali zetu. Huwezi kwenda dukani umevaa t-shirt ama kofia ya chagua Magufuli bei ya sukari ikapungua, sio sukari tu... bidhaa yoyote ile watu wa CCM nao wanaisoma namba sawa na sisi wa upinzani.
Pumbaaaaafu zenu, hata ule wimbo wa CCM mbele kwa mbele siku hizi umetupunguzia kelele hapa mtaani kwa jirani yetu, kutwa alikuwa akiupiga mara nane na zaidi, najiuliza... sijui ameuza ile flash yake. Ila nahisi ni kwa sababu na yeye amechoka kuzisoma hizi namba, maana ni ndogo zinahitaji miwani.
Leo hii ukipita mitaani hasa vijiweni, unawasikia watu wa CCM wanaitetea CCM kwa mbinu ile ile kwamba, hapana... CCM kama chama hakina tatizo, ila tatizo ni mtu amekuwa na maamuzi tofauti na malengo ya chama chao.
Mimi huwa nawauliza kuwa, hivi wamesahau uchaguzi uliopita waliwaaminisha watu kuwa wanamchagua mtu safi, huku wakiiweka CCM kando. Rejeeni kauli mbiu ya kampeni "Chagua Magufuli" badala ya "Chagua CCM".
Francis M. Garatwa,
Diwani kupitia CHADEMA.

Maoni