WATANZANIA 67% WAITAKA KATIBA MPYA WAKATI MAGUFULI ANASEMA SIO KIPAUMBELE CHAKE.

Utafiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza umebainisha kuwa asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu Tanzania kupata katiba mpya, asilimia 56 wanasema toleo la mwisho la rasimu ya katiba lipigiwe kura na wananchi, huku asilimia 48 wakisema katiba mpya haiwezi kupatikana ndani ya miaka mitatu
Hii ni mara ya nne tangu taasisi ya Twaweza ianzishe utafiti unaohusisha maoni ya wananchi juu ya katiba kutokana na matukio mbalimbali wanayoyashuhudia na kuyasikia ambapo asilimia 91 ya wananchi wanakubali kuwa mchakato wa kuunda katiba na maudhui yake vyote ni muhimu
Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze anasema asilimia 93 ya wananchi wamewahi kusikia kuhusu katiba, asilimia 35 wanaeleza maana ya katiba na asilimi 49 wanasema rais ndiye anayepaswa kuongoza mchakato wa kubadilisha katiba.
Matokeo ya utafiti huo yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa elfu moja mia saba na arobaini na tano katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara kuanzia mwezi Juni hadi Julai mwaka huu
FacebookTwitterGoogle+

Maoni