Wakati Tanzania imejitoa katika Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP), sababu za kufanya hivyo zimebainika.
Barua ya Tanzania kujitoa katika mpango
huo iliyoandikwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga ya Juni 29
iliyowekwa kwenye tovuti ya OGP imeeleza sababu ni kutokana na kuwepo
kwa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2016.
Amesema sheria hiyo inalenga kuongeza haki ya upataji wa taarifa na uwazi wa shughuli za Serikali.
Sababu nyingine amesema ni Serikali
kuanzisha Tovuti Kuu ya Takwimu Huria (www.opendata.go.tz) kuchapisha
data ili zitumiwe na mtu yeyote na hasa kutoka sekta za kipaumbele za
elimu, maji na afya.
Pia, amesema Tanzania ni mwanachama wa Mpango wa Afrika wa Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) wenye malengo sawa na OGP.
Kutokana na hilo, amesema Tanzania inaamini uanachama katika mpango mwingine wenye malengo sawa unaweza kuathiri ushiriki wake.
Tanzania ilikuwa mwanachama wa OGP tangu
Septemba 2011. Dhamira ya Serikali kujiunga na OGP ilikuwa kufanya
shughuli zake kuwa wazi zaidi kwa wananchi kwa manufaa ya uboreshaji wa
utoaji wa huduma kwa umma katika kupambana na rushwa na kujenga uaminifu
zaidi.
Maoni
Chapisha Maoni