WATANZANIA WASHINDWA KUMWELEWA KAMANDA SIRRO NI IGP WA POLISI AU MWANASIASA KWA KAULI.



NARUDIA TENA; IGP SIMON NYAKORO SIRRO.., Twende kwa falsafa za kutenda kazi kwa weledi.., tuache kufanya shughuli za polisi kwa taswira yenye ukinzani wenye kuacha madoa....
SIRRO KWENYE MTANZIKO WA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI
Sirro umesema watu kadhaa ambao walikamatwa kwa kuhusishwa kwenye tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi 07—09—2017 huko Dodoma wameachiwa baada ya Mahojiano..., Unakwenda mbali na kusema unamtaka dereva wa Lissu ajisalimishe ili upelelezi uendelee....
Sirro wewe ni mtaalam wa sheria.., pia mbobezi wa shughuli za upelelezi ambazo umezifanya kwa muda mrefu, kwamba Unataka kusema na kutuaminisha kwamba dereva wa Lissu ndie 'prime suspect' hadi sasa!? Kwamba ndie ambae anaendelea kukwamisha shughuli za upelelezi wa tukio hilo!? AU...
Sirro, katika kozi ya sheria kama zilivyo kozi nyingine nyingi.., wasomi wanafundishwa saikolojia ya binadamu.., unataka kusema haujui kabisa athari za kisaikolojia ambazo dereva wa Lissu anaweza kuwa amezipata katika tukio hilo la ndugu yake kupigwa risasi nyingi mbele yake!? AU.....
Kwamba leo unashangaa kumuona dereva wa Lissu akiwa amenawiri na kuchanua!? Ulitegemea kumuona akiwa kwenye hali gani? Amechakaa!? Umeelezwa yupo kwenye tiba ya kisaikolojia.., hayo ambayo unayaona kwake ndio mafanikio ya tiba.., ndio maana wenzake waliona ni vyema kumpeleka Nairobi kwenye tiba..
Unasema dereva wa Tundu Lissu akionekana., atawasaidia kupata majibu ya maswali mengi...., wakati huo unasema waliokamatwa awali wameachiwa huru baada ya Mahojiano kukamilika.., hivi unaweza vipi kuwaachia huru watuhumiwa wa Shambulio la mauaji kwa silaha za moto ikiwa aliyeshambuliwa yuko hai na anaweza kutumika kuwatambua!? Sijaelewa mantiki katika hilo...
Katika hili la Lissu pia Sirro unasema Lissu ni mtanzania kama watanzania wengine na unasema wanaopigwa risasi ni wengi..., Sawa, ni kweli kabisa Lissu ni mtanzania kama wengine lakini swali langu ni kwamba.., kwa sababu wanaopigwa risasi ni wengi basi hatupaswi 'kushadadia' tukio la kupigwa risasi mchana wa Jua kali kwa mbunge, mwanasheria wa CDM, mnadhimu wa KUB, Rais wa TLS!? AU unataka kusema nini!??
DEREVA WA TUNDU LISSU;
Dereva wa Tundu Antiphas Mughwai Lissu anaitwa Simon Mohammed Bakari yuko Nairobi kwa sasa.., hizo porojo za awali kwamba ametoweka na hataki kuonekana ni ujinga wa kupuuzwa..., yuko Nairobi akiendelea na huduma za kisaikolojia, yupo kwenye mikono salama.., alishuhudia tukio na kuokoka kimiujiza.., kutokana na hali ya usalama wa maisha yake ilikuwa lazima apelekwe nje ya mipaka..., kwa aina ya shambulizi lile, jamaa walitaka kuondoa uhai wa wote wawili..., Mungu ni mwema sana.., siku zote na hata milele.., they survived to tell the tale...
Naendelea kuamini kwamba, dereva wa Tundu Lissu ambae ni first physical witness lazima atohojiwa.., na lazima atatoa ushirikiano wake kama ambavyo alijitahidi kumsaidia Lissu kabla na baada ya kupigwa risasi.., hivyo lazima atatoa ushirikiano wake.., kwa uhitaji huu wa polisi, mnaonesha umma kwamba dereva wa Lissu ni Prime suspect kwenye issue hii.., amekuwa dereva wale tangu Lissu anawaeleza kufuatiliwa na ameendelea kuwa dereva wake hata siku ya kupigwa risasi na sasa wako wote Nairobi.., atakuja, lazima afike.., but Lissu yupo hai na atasema yote.., atamtaja kama ni mhusika.. Acheni kufinyanga hili suala..
NAENDELEA KUKAZIA MAARIFA;
Yes, kwenye tukio la Tundu Antiphas Mughwai Lissu kushambuliwa kwa risasi na 'unknown pre—mature creatures' .., lazima waliokuwa kwenye 'crime scene' wahojiwe na vyombo vya usalama.., hata Tundu Lissu akipata nafuu na kurejea kwenye hali yake nae atahojiwa.., ndivyo ilivyo.., na ulimwenguni kote CI's process zinafanana..
Lakini, crime scene investigators (CSIs) and Law enforcers wanafahamu namna sahihi ya kuendesha criminal investigations.., 'non—disclosing' the evidence, suspects, perpetrators, witnesses ni muhimu sana kwenye upelelezi wa makosa ya jinai.., kutangaza hadharani kwamba unamtaka Dereva wa Lissu ajisalimishe polisi kwa mahojiano ni kinyume kabisa na code and ethics/principles of crime scene investigation.
.., kwa taswira ya tukio husika.., hata huyu dereva alipaswa kupewa ulinzi na usalama wa maisha yake.., pia kwa sababu ameshuhudia tukio la mtu wake wa karibu.., hakuna sababu za kwanini aitwe siku ya pili baada ya tukio kubwa la uhalifu wa maisha ya binadamu kwa kupitia vyombo vya habari tena hadi sasa mmeendelea kushupaa.., sikutaka kuamini kama angelitoa ushirikiano wa kutosha kwa nyakati zile.., labda sasa anaweza.., anahitaji utulivu wa mwili, akili na mengineyo.,
., nafikiri, upelelezi uendelee kama kawaida., lakini kwa kuto' disclose ( Non-disclosure) suspects, perpetrators, witnesses na physical evidence.., tusitumie vyombo vya habari kuitana kwenye upelelezi wa polisi na kutaja yupi anatakiwa na yupi ameachiwa., bado tension ni kubwa sana kwenye jamii., kumbuka hii ni drive—by shooting scenario.., tusiweke uhai wa wengine rehani., ni ushauri wangu hafifu tu.. 
 #ButWhatDoIKnow
—————————————
© Martin Maranja Masese (MMM)

Maoni