BAADA YA USHAHIDI WA NASSARI JUU YA MNYETI KUTOA RUSHWA KUWA KIMYA MPAKA LEO TAKUKURU WAMEKUJA NA NYALANDU BAADA YA KUAMA CCM.

 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema kuwa imeanza kulifanyia kazi agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangalla la kumchunguza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali,  John Mbugo alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari, ambapo amesema kuwa endapo wakimkuta Nyalandu ana hatia watamfikisha panapostahili

Aidha, Dkt. Kigwangalla  akiwa bungeni hapo jana wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/18 aliagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu kwa madai kuwa aliisababishia serikali kukosa mapato na tuhuma zingine zenye kuhusisha rushwa.

 Hata hivyo, kwa upande wake, Nyalandu kupitia mitandao ya kijamii amekuwa akikanusha tuhuma alizoelekezewa kwake na waziri huyo na kusema kuwa hizo ni tuhuma zenye lengo la kumchafua pamoja kuwaogopesha watu wengine wenye nia ya kuhama Chama Cha  Mapinduzi (CCM)

Maoni