DARASA LA UJASILIAMALI KUTOKA KWA YERICKO NYERERE KWA WATANZANIA.

Darasa la Ujasiliamali kwa waswahili wenzangu tu, isipokuwa wale wa masaki na mikocheni wanaolindwa na Sheria ya habari na Saibakilaimu hapa hapawahusu kwakuwa wao wanaurithi kwa jasho la mtanzania.
Ukipata wazo la kuhitaji kuingia katika Shughuri Yoyete ile ya Ujasiliamali Mkubwa au Mdogo, Fanya Haya Yafuatayo Kabla Ya Kujitosa.
1). Fanya Utafiti Wa Biashara Husika Ili Ujue Lugha Ya Bidhaa Yako, Faida, Changamoto Na Mengineyo.
2). Mtafute Mtu Wa Mwaminifu Wa Kukushika Mkono (Mentor) Ili Akuonyeshe Mlango Wa Kuingilia Na Wakutokea, Dhumuni Ni Kupata Uzofu Na Mbinu Mbadala Za Kufikia Malengo Yako.
>Ifahamike Kwamba Huwa Ni Ngumu Kidogo Kumpata Mentor Wa Kukuongoza Maana Ni Jambo Linalohusisha Mgongano Wa Kimaslahi So Huleta Hofu Kwa Wengi Wanaofanya Biashara Kama Unayotaka Kuifanya.
>Unaweza Pia Kuongea Na Waajiriwa Au Watu Ambao Walishawahi Kufanya Biashara Hiyo Then Wakaiacha Kwa Namna Moja Ama Nyingine.
3). Baada Ya Mambo Yote Hapo Juu, Unaweza Kuanza Kufanya Uwekezaji Wako Lakn Ni Vyema Ukaanza Kwny Msimu Ambao Bidhaa Yako Inapatikana Au Inatoka Kwa Urahisi Ili Tu Kuepuka Ushindani Na Wazofu Wa Biashara Husika.
>Fanya Hivyo Hata Kama Mtaji Wako Ni Mkubwa Kuliko Wazoefu Maana Wazoefu Wana Mbinu Nyingi Sana Za Kuweza Kukuangusha Ktk Msimu Ambao Bidhaa Hupatikana Kwa Nadra Sana Wakat Mahitaji Yako Juu Sokoni. Kumbuka Kuwa Wazoefu Wana Wigo Mpana Hata Kama Mitaji Yao Ni Midogo Maana Network Yao Ni Kubwa Sana Kuanzia Shambani Hadi Sokoni Tofauti Na Mjeni Kama Wewe.
Mfano> Subiri Maembe Yawe Yanapatikana Kwa Urahisi Ndio Uanze Biashara Yako Ili Uwekeze Mtaji Mdogo Bila Kujali Faida Kubwa Sana Kwa Dhumuni La Kupata Uzoefu Zaidi Na Zaidi Na Kujiandaa Kujiongoza Mwenyewe Kwenye Msimu Mgumu.
*Shughuri Zote Za Kiuchumi Zinahitaji Utafiti Yakinifu Ili Kutengeneza mpango wa kibiashara mzuri ambao utaleta Matokeo Chanya Kwenye Uwekezaji Wako.
>Wengi Wetu Hatupendi Kufanya Utafiti Kwa Kukwepa Gharama Lakn Tumesahau Falsafa Isemayo Kuwa "Utafiti Ni Hasara Lakini Ni Faida."
Utafiti Unatoa Mwanga Wa Uelekeo Wa Biashara Yako Hata Kabla Hujaanza Kuifanya Licha Ya Kwamba Unagharama Za Hapa Na Pale.
Wengi Wanapotaka Kuanza Ujasiliamali Wanawaza Faida Tu Lakini Hawajui Au Wamesahau Kwamba Faida Ni Matokeo Au Jambo La Mwisho Kabisa Baada Ya Mambo Yote Kufanyika Tena Kwa Ufasaha.
Mimi Sioni Kama Ni vema Kwa Mtu Kuendelea Kuajiriwa Kwenye Ajira Ambayo Hata Yeye Mwenyewe Anauwezo Wa Kuwekeza Kimtaji, au taaluma aliyonayo inamuwezesha kujiajiri, Ana Uzoefu, Fikra Pevu, Anajua Changamoto Na Mengneyo.
Unaweza Kuajiriwa Kwa Maana Ya Kutafuta Uzoefu Katika Biashara Husika Ama Kutafuta Mtaji Lakini Mwisho Wa Siku Andaa Mazingira Ya Kujiajiri Mwenyewe. Usiwe Mtumwa Wa Kufanya Kazi Za Watu Wakati Malipo Ni kidogo Na Mazingira Ya Kazi Ni Magumu na kutumbuliwa kuko njenje kama mate ya mjamzito.
Kama Ni Mama Lishe, Basi Anza Kununua Kifaa Kimoja Kimoja Kama Vile Jiko, Sufuria Na Mahitaji Mengineyo Then Ukikamilisha Vyote Sasa Unaweza Kuacha Ajira Na Kujiajiri.
>Kumbuka Kuwa Na Mtaji Wa Kulinda Biashara Yako (Working Capital) Ili Uweze Kutatua Shida Ama Matatzo Yanayojitokeza Papo Kwa Papo Kwa Mahitaji Yaliyopelea.
Jiamini Na Usiwe Mapepe Maana Kutengeneza Wateja Si Jambo Rahisi Sana Japo Liko Ndani Ya Uwezo Wako Wewe Mwenyewe.
ASIKUDANGANYE MTU.
Hakuna Biashara Rahisi Chini Ya jua Ila Penye Ugumu Kuna Mafanikio.
>Hakuna Biashara Mbaya Chini Ya Jua Labda Ile Ambayo Imekatazwa Kisheria Au Ktk Maandiko.
>Hakuna Biashara Isiyo Na Faida Na Wala Hakuna Biashara Isiyo Na Hasara.
>Faida Na Hasara, Vyote Ni Haki Ya Mjasilimali.

NGOJA NIKUKUMBUSHE MSWAHILI MWENZANGU.
>Kamwe Huwezi Kupata Faida Ama Hasara Bila Uthubutu. Uthubutu Ndio Njia Ya Mafanikio Ama Kufeli Lakn Pia Uthubutu Ndio Unamfanya MjasiriaMali Kuwa Jasiri Na Kufikia Malengo Yake.
ZINGATIA: UTAJIRI HUJA KWA WENYE KUIFUATA HOFU WAKATI UMASIKINI HUENDA KWA WENYE KUIKWEPA HOFU.

Maoni