HOTUBA YA NYALANDU MTWARA YAKWAMISHWA NA NDEGE YA KWENDA MTWARA.
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
ambaye hivi karibuni amekihama chama cha CCM na kujiunga na CHADEMA,
ameshindwa kupanda jukwaani na kuhutubia mkoani Mtwara kama ambavyo
iliarifiwa na uongozi wa CHADEMA.
Akithibitisha hilo mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
wa Chadema, John Mrema amesema kuwa kukosekana kwa ndege inayofanya
safari kati ya Dar es Salaam na Mtwara kumemsababishia Nyalandu
kushindwa kuhudhuria mkutano huo, kwani alikuwa Nairobi nchini Kenya
kumjulia hali Tundu Lissu.
Amesema kuwa Nyalandu amefika Dar es Salaam na kukosa ndege ya kwenda
Mtwara, hivyo amewaomba radhi wananchi ambao walikuwa wanasubiria
kumsikiliza na kwamba wanaandaa kwa ajili ya siku nyingine kuweza
kufanya hivyo.
“Tunaomba radhi kwa hili ila tukio hilo tunaliandalia mahali pengine na wakati ukifika tutakuwa pamoja naye,”amesema Mrema
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Jumamosi akihutubia
mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata
ya Saranga jijini Dar es Salaam alisema amempokea Nyalandu na Jumapili
Novemba 12, 2017 angeungana naye kwenye mkutano wa kampeni mjini Mtwara
Maoni
Chapisha Maoni