Ruka hadi kwenye maudhui makuu
KAMATI MBILI ZAUNDWA KUSHUGHULIKIA SEKTA YA GESI NA UVUVI NA SPIKA WA BUNGE NDUGAI
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameunda
kamati mbili zitakazoshughulikia sekta ya Uvuvi na Gesi ili kuweza
kujua ni kwa nini hazichangii pato la taifa.
Ndugai ameunda kamati hizo baada ya zingine mbili za kutathmini mfumo
wa uchimbaji, usimamizi. umiliki na usimamizi wa madini ya Tanzanite na
almasi kuwasilisha taarifa kwa Rais Dkt, John Magufuli na kusababisha
baadhi ya mawaziri kujiuzulu.
Akitangaza kamati hizo bungeni mjini Dodoma, Ndugai amemrejesha Dotto
Biteko aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyochunguza madini ya Tanzanite
kuwa mwenyekiti wa kamati itakayochunguza sekta ya gesi.
Amesema kuwa hali ya kusuasua katika sekta hizo unahitaji kufanyiwa
utafiti ili kuweza kuona ni namna gani zitaweza kuchangia pato la taifa.
Hata hivyo. Ndugai amemuagiza Katibu wa Bunge kuwawezesha wabunge hao
ili waanze kazi mara moja na kamati hizo zimetakiwa kufanyakazi ndani
ya siku 30 tangu zilipokabidhiwa majukumu.
Maoni
Chapisha Maoni