Makamu wa rais aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa amtaka Mugabe ajiuzulu mara moja
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Makamu wa rais wa zamani , ambaye
kufutwa kwake kazi kulisababisha jeshi kuchukua mamlaka ya nchi ,
amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja.
Emmerson Mnangagwa amesema alitoroka nje ya nchi wiki mbili
zilizopita wakati alipobaini kuwa kuna njama za kumuua na hatarejea
nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wake.
Afisa
wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa
bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua
siku mbili tu.
Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na
kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya
kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''
Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua
mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani
aliyeuhamishoni karibuni.
Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.
Mugabe ''alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba
Mugabe
''alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba, licha ya shinikizo kubwa Bwana
Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika
hotuma yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa
chama Zanu-PF.
Maoni
Chapisha Maoni