Moto wazuka kituo cha habari cha Clouds Media Group nchini Tanzania
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Jeshi la zima moto limefika katika
jengo la kituo cha habari cha Clouds Media Group jijini Dar es salaam,
kudhibiti moto uliozuka katika mojawapo ya vyumba vya kurushia matangazo
ya televisheni.
Tayari moto umeshadhibitiwa.
Sebastian
Maganga, mkuu wa maaudhui na uzalishaji wa Cloud Media Group, ameiambia
BBC kwamba, "moto umetokea kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nne ,
athari saizi ni vigumu kuzijua. Eneo ambalo limeungua ni chumba cha
kurushia matangazo ya televesheni."
Mojowapo ya vipindi vilikuwa vikuruka hewani hapo ambapo moto ulipozuka.
Pia Ambwene Mwakibete, Kaimu Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji, mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, amesema kwamba
"Tumeidhibiti
moto ili usimbae kwenye vyumba vingine. Tumeona ni mfumo wa kiyoyozi
ambao ni umeme ndio tumeona umeathirika kwa sehemu kubwa."
Hamna majeruhi wala vifo, na thamani ya uharibifu haijafahamika bado. Chanzo cha moto hadi sasa bado hakijafahamika.
Maoni
Chapisha Maoni