NDIKUMANA MUME WA UWOYA AFARIKI DUNIA AKIWA NCHINI RWANDA

 


Habari ya kusikitisha, mume wa zamani za Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia. Alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda. 

Uongozi wa timu hiyo umesema jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya.

 Mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajafanya ajali. Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake kwani miili ya waislamu haihifadhiwi katika monchwari za kawaida kwa mujibu wa imani zao. 

Mungu ampe malazi mema peponi. 



 

Maoni