Ruka hadi kwenye maudhui makuu
POLISI WAPIGA MABOMU NA KUSIMAMISHA MSAFARA WA NAIBU KATIBU MKUU MNYIKA VITU VIMEPOTEA SIMU ,PESA NA VINGINE.
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA - Bara *Mhe. John J. Mnyika* leo Novemba 19,
2017 ameongea na wakazi wa Momba katika mkutano wa kumnadi Mgombea
Udiwani kupitia CHADEMA katika uchaguzi wa marudio katika Kata hiyo ya
Ndalambo iliyopo wilaya ya Momba mkoani Songwe.
Mkutano huo
ambao ulishirikisha Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwemo Wabunge Mhe.
Ernest Silinde - Mbunge wa Momba, Mhe. Frank Mwakajoka - Mbunge wa
Tunduma na Mhe. Risala Kabongo - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe
ulimalizika kwa polisi kuzuia msafara wa Viongozi hao na kuanza kupiga
mabomu ya machozi ovyo.
*Updates kuhusu mabomu yaliyorushwa kwenye msafara wa Mnyika na gari lake lililochukuliwa na Polisi...*
Baada ya Polisi kupiga mabomu msafara huo na baada ya kumpiga dereva wa
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA walitoa vitu vyake kwenye gari
zikiwemo nyaraka mbalimbali na mabegi na kisha kuondoka na gari lake
jambo lililolazimu Mhe. Mnyika pamoja na Viongozi wengine kuelekea Kituo
cha Polisi Tunduma kwa ajili ya kufuatilia suala hilo ambapo mpaka sasa
gari limeshakabidhiwa kwa Viongozi hao wa CHADEMA lakini Mhe. Mnyika
ajaona simu zake mbili ambazo zimepotea pia kufuatia tukio hilo kuna
upotevu wa Shilingi laki nane (800,000/=) za Kitanzania pia Dereva wa
Naibu Katibu Mkuu John Mnyika aliyetoweka baada ya kuwakimbia Polisi
waliokuwa wakimdhibiti tayari ameshajitokeza.
Taarifa zaidi tutazidi kuwaletea...
Habari CHADEMA
Kanda ya Nyasa
Maoni
Chapisha Maoni