TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TANESCO:Upungufu wa umeme baadhi ya maeneo, jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa
leo Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017 kuna
usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I,
sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo
cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.
Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya
Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa
maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme. Zoezi hilo
linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme
kwa wakati.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za maendeleo ya kazi. TAHADHARI
Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo
ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji
vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili
kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika
maeneo yaliyo karibu na Mitambo. Shirika limesha fanya taratibu zote za
ki usalama katika eneo la Mitambo.
Maoni
Chapisha Maoni