UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NCHINI TANZANIA UMEJAWA VURUGU KUTOKA KWA CCM WAKILINDWA NA VYOMBO VYA DORA NA WATU KUSEMA AMNA HAKI YA KUCHAGUA PIA VYOMBO VYA HABARI MBALIMBALI VIMESHINDWA KUTOA HABARI.

 

Wakiwachokoza wapigeni bila huruma. Polisi na magereza ni vyetu, msiogope" Laerence Masha & Hussein Bashe, 24/11/017. Asanteni kwa maagizo yenu ambayo yametekelezwa vizuri na wanachama wenu, lakini msisahau kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi. Laiti mngejua kuwa utaifa wetu ni muhimu kuliko vyama vyetu, msingeropoka mliyoropoka. Damu hizi zikanene juu yenu, kama inenavyo damu ya Habili.!

 1. Mawakala wote wa Chadema kata ya Mamba katika vituo 13 wameondolewa kwa amri ya polisi. Uchaguzi unaendelea kwenye kata hiyo bila kuwepo kwa mawakala.

2. Vijana wa CCM wenye gari nambari T 733 AHH, Toyota Prado, rangi ya blue wakiwa na mapanga, mawe, nondo na visu wamekamatwa wakiwa wanazunguka kata ya Muriet. Hata hivyo walifanikiwa kutokoroka kabla hawajachukuliwa hatua.

3. Mkuu wa wilaya ya Arusha, akiwa kwenye gari yenye namba T 348 AFE, Toyota Labdcruizer, amefukuzwa na wananchi kata ya Muriet alipojaribu kuvikabili vikosi vya ulinzi vya Chadema.

4. Meya wa Ubungo ambaye ni Wakala Mkuu kata ya Saranga, Boniface Jacob amekamatwa na Polisi mchana huu.

5. Mgombea udiwani kata ya Bomambuzi Moshi kwa tiketi ya CCM Juma Rahibu amenusurika kupokea kipigo kutoka kwa wananchi, kabla ya kuokolewa na polisi. Mgombea huyo akiwa na vijana wenzie wa CCM walimvamia diwani wa Mfumuni Bw.Tonny Ndewawio (Chadema) na kumjeruhi kwa mapanga siku chache zilizopita.

6. Matukio ya utekaji nyara, utesaji na mashambulizi ya kutumia silaha yameendelea kushamiri katika kata mbalimbali nchini zinazofanya uchaguzi wa Marudio. Kata ya Muriet mgombea Udiwani wa CCM Samson Laizer akiwa na vijana wa CCM wamejeruhi mawakala wa Chadema kwa mapanga, bisibisi, nondo na marungu. Majeruhi kadhaa wamekimbizwa ICU Mt.Meru Hospital.

7. Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega amekamatwa na jeshi la Polisi katika kata ya Kimala, mkoani Iringa, kwa madai ya kufanya siasa kwenye kata isiyo yake.

8. Kada wa Chadema kata ya Mamba (pichani chini) amevamiwa na viongozi wa CCM na kuvunjwa mkono, kupigwa nondo sehemu za mbavu, na kuchomwa na bisibisi kichwani.

9. Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Lawrence Masha na Mbunge wa Nzega Hussein Bashe wamewataka wanachama wa CCM kuwapiga bila huruma wanachama wa Chadema watakaowachokoza. Katika kuweka msisitizo wa kauli hiyo, wamewataka wanachama wa CCM wasiogope kwa kuwa jeshi la polisi na jeshi la magereza vipo chini yao.

10. Mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe.Freeman Mbowe ametangaza chama chake kujitoa kwenye uchaguzi wa kata 5 za Arumeru kufuatia vitendo vya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi, na mawakala wa Chadema kuvamiwana na kujeruhiwa na makada wa CCM. Mbowe ametoa wito kwa wanachama kujilinda.

Maoni kutoka kwa Mwanaharakati wa chadema  Malissa G

Maoni