UHUSIANO WA KENYA NA TANZANIA SASA UNAENDA SEHEMU MBAYA WAKATI TUPO KATIKA EAC.


Kenya imewasilisha malalamiko rasmi kwa Tanzania, kuhusiana na kile serikali mjini Nairobi, inachokieleza kuwa "mabadiliko ya Kisera" yanayopuuza vitendo vya uhasama dhidi ya raia wa Kenya na maslahi yao ya kibiashara. Hii inafuatia kitendo cha kuteketezwa vifaranga 6400 vilivyoingizwa nchini Tanzania pamoja na tukio jingine la kupigwa mnada hivi karibuni ng'ombe kiasi 1325 kutoka Kenya. Kenya imemuita balozi wa Tanzania Nairobi kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo waziri wa mifugo na Uvuvi wa Tanzania Luhaga Joelson Mpina anasema ng'ombe waliopigwa mnada hawana mwenyewe na hatua walizozichukua zinazingatia sheria ya Tanzania.

Maoni