UJUMBE MZITO KUTOKA KWA MWANAHARAKATI KWENDA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA MBOWE.

 

Mwenyekiti wetu Freeman. Lissu yupo kitandani, Mawazo, Mwangosi wapo ardhini, Ben hatujui alipo wengi wengine yawezekana wamefanyiwa haya na hatujui.

Mwenyekiti wewe binafsi na wenzako mmepambana kwa Miaka 25 wengine tukiwa wadogo hadi Leo tumekua na tuko na wewe bega kwa bega ukihubiri demokrasia, haki utawala wa sheria kwa njia zilizopo katika katiba yetu.

Mwenyekiti tupo katika utawala wa awamu ya tano ulioamua kwa dhati kujitia upofu wa demokrasia, utawala wa sheria, uvunjaji wa katiba na kuvaa roho ya unyama dhidi ya utu wa watu wetu.

Mwenyekiti ni dhahiri sasa serikali ya awamu ya tano chini ya mwenyekiti wake wamezidiwa kwa mbinu tulizokuwa tunatumia kwa miaka 25 na sasa wameamua na kuja na mbinu moja ya kufuta upinzani kwa mabavu, silaha, utekaji na mbinu za kijeshi.

Mwenyekiti kwa tafsiri ya matukio haya si kuwa tunapaswa kufikiri mbinu mbadala nje ya boksi la kura na demokrasia bali tunalazimishwa kufikiri na kutenda nje ya njia za siasa safi. Mwenyekiti tunalazimisha kujua asili ya gwanda si lile linalopaswa kubeba kitambulisho cha kubeba kura bali vifaa mbadala sawa na vile walivyobeba wazee wetu wa majimaji na mau mau.

Mwenyekiti hakuna sisi wanasiasa na umma ambacho wadhalimu hawajatufanyia. Tayari damu na dhuluma nyingi zimefanyika, roho nyeusi si unapenda kuivaa ila ndio iliobaki ili tuvuke, damu na Mali za kutosha tumesha poteza.

Mwenyekiti tujitazame upya kuokoa demokrasia ya nchi yetu, tujitazame sisi tuliobeba mamlaka, nadhani matamko ya kulaani na kukemea yanatosha, wazee wa chama na viongozi wetu wasiokuwa tayari kubeba huu ujasiri watupishe. Mwenyekiti hapa tulipo ni rahisi na pagumu, urahisi ni kubadili mbinu tuu na kuvaa roho wanayotukabili nayo na ni pagumu kama tutavaa roho ya matamko na kulaani.

Damu zilizomwagika basi ni wakati muafaka kuandika historia ya ukombozi na ukombozi huu wa udhalimu wa CCM ni lazima ufike kikomo kwa damu ya haki kutetea haki dhidi ya damu ya dhuluma.

Sioni kificho, hofu wala woga kusema siasa ya sasa si ya Mic au mayowe maana tayari umma ushafanya maamuzi ila unatiwa hofu. Sasa tuutoe hofu umma huu tuwavushe, tuwaeleze namna ya Kubeba vifaa vya ukombozi, tujue hii ni vita dhidi ya CCM na vyombo vyake vya ulinzi.

Vijana wenzangu wa CHADEMA na wapenda haki tutamalizwa mmoja mmoja hadi lini? Tutasubiri hadi lini kujilinda na kushambulia tukitegemea Police watulinde? Ifike mahali tujue kupitia kauli za Bashe na Masha kuwa sisi ni yatima hatuna Jeshi la polisi , magereza nk ingawa tunalipa kodi. Niwakati wa kujua kuwa tunapaswa kulivusha taifa, kuilinda demokrasia, nchi yetu, haki na chama chetu. Sosopi Ndio kiongozi wetu kwa vijana najua unajua lugha ya vijana usihofu kuinena. Kama wanatupiga mapanga , Mawe na bado tunashikwa sisi nadhani vijana wenzangu tuzungumze katika lugha yao.

Nimalize kwa kuwaambia wapenda mabadiliko hakuna tena kukubali haya yaliotokea leo katika uchaguzi wa kata zetu ni dalili za matukio 2020 CCM watafanya. Tujiandae kushika dola kwanjia yeyote ile sawa au zaidi ya njia ambayo CCM itakayotumia kujilinda. Nia tunayo, dhamira tunayo na nguvu pia tunayo ya Kuilinda haki, demokrasia na mabadiliko hata kwa zana za jadi za kilimo cha jembe la mkono.

H.A
Mwanamabadiliko.

Maoni