VIONGOZI WA CHADEMA WASEMA CCM PAMOJA NA VYOMBO VYA USALAMA NCHINI WANATUMIA NGUVU KUBWA KUHARIBU UCHAGUZI WA UDIWANI NCHINI BAADA YA KUONA WANASHINDWA.









Mawakala wa Chama wote wametolewa nje ya vituo vya kupigia kura kata zote tano za jimbo la Arumeru Mashariki
Wanasema sababu ni kwamba fomu ya Wakala ilipaswa kusainiwa na msimamizi wa jimbo Na siyo msimamizi msaidizi.
Cha ajabu ni kwamba sheria inaruhusu Wakala kuhapishwa Na msimamizi,msimamizi msaidizi Na mawakala wote wameapishwa Na wasimamizi wasaidizi kwenye kata alafu wa nataka kuwepo Na saini ya msimamizi mkuu wa jimbo?? How comes?
Hakika hii ni mbinu chafu yakuihujumu Chadema,Na demokrasia ndani ya nchi hii.
Ni vyema kama serikali ya Ccm haitaki tena ushindani wa vyama vingi wakavifuta kabisa.
Wametutoa wote nje ila wao wanajua ninikitaendelea kwani wanaohusika Na kutatua tatizo hili hawapatikani.
Na Mimi mwenyewe Jana jioni niliwasiliana Na mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya uchaguzi Taifa akanijibu kuwa yeyote kati yao anaweza kuapisha bila shida.
G.mwanda m/kiti Chadema w.Meru.

Maoni