Ruka hadi kwenye maudhui makuu
WABUNGE CUF WAMUANDIKIA BARUA SPIKA KUTAKA UTEKELEZWAJI WA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU ILI WAENDELEE NA UTENDAJI KAZI WAO.
WABUNGE CUF WAMUANDIKIA BARUA SPIKA KUTAKA UTEKELEZWAJI WA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU:-
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
KUHUSU MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA
DAR ES SALAAM KUREJESHWA KATIKA NAFASI YA UBUNGE
WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1. Ndugu Waandishi wa Habari; Awali ya yote hatuna budi kumshukuru
Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia Uzima na Afya njema ya kuweza
kukutana hapa leo kuweza kuzungumza nanyi na kupitia nyinyi kufikisha
ujumbe wetu kwa Watanzania wote.
2. Mtakumbuka kuwa Tarehe
25 Julai, 2017 Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania,
Mheshimiwa Job Ndugai, alitangaza kutuvua Ubunge Wabunge [8] wa CUF Viti
Maalum kwa kasi tuliyoiita (supersonic speed) na baadaye haraka haraka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] kuwatangaza wafuasi wa Lipumba kuchukua
nafasi hizo bila ya kufuata utaratibu huku wakijua kuwa kuna Shauri
Mahakamani linalosubiri kusikilizwa na kufanyiwa maamuzi.
3.
Tulifungua Shauri la Madai Mahakama Kuu ya Tanzania (Civil Case No.
143/2017) na Shauri dogo la Madai (Miscellaneous Civil Case No.
479/2017). Hata hivyo, kutokana na michakato ya kisheria Mahakama Kuu
haikuweza kutoa maamuzi ya Zuio [Temporary Injunction and Maintenance of
Status Quo] tuliloomba kwa wakati huo ndani ya muda muafaka. Baadaye
Tarehe 5 Septemba, 2017 Wafuasi 8 wa Lipumba waliotangazwa kuwa
wameteuliwa na NEC kuwa Wabunge waliapishwa na Bunge kuchukua nafasi
zetu.
4. Tarehe 10 Novemba, 2017 Mahakama Kuu baada ya
kusikiliza maombi yetu na kuzipitia hoja za pande zote imetoa maamuzi ya
kuizuia CUF kujadili kwa namna yoyote ile Uanachama wetu na imetengua
utekelezwaji wa kufukuzwa kwetu Uanachama (suspend implementation),
kisheria ikiwa na maana kwamba sisi sote bado ni Wanachama halali wa CUF
na pia bado tuna sifa za kuendelea kuwa Wabunge.
Sehemu ya Maamuzi ya Mahakama Kuu inasomeka kama ifuatavyo, ninanukuu:
“…The object of the temporary injunction is to protect the plaintiff
against injury by violation of his right for which he could not
adequately be compensated in damages recoverable in the action if the
uncertainty were resolved in his favour on the trial…”
To the
extent it relates to the 1st, 2nd, and 3rd Respondents, it can hardly be
argued in this application that a loss shutting down the Applicants
political carrier can be easily atoned by award of damages and I would
not hesitate upholding the submission on the second principle.
Lastly, on balance of convenience. Under this condition, the court has
to assess in whose favour the balance lies by the grant or refusal of
the order sought. Again I am Satisfied that the Applicants have met this
condition. The Applicants have averred that have appealed to the
MKUTANO MKUU against their expulsion from CUF and that pending the
determination of their appeals, the 1st, 2nd, and 3rd Respondents should
be restrained from implementing their impugned decision.
“….IN
ZITTO ZUBEIR KABWE V. BOARD OF TRUSTEES OF CHAMA CHA DEMOKRASIA NA
MAENDELEO & ANOTHER, CIVIL CASE NO. 270 OF 2013 (unreported) this
Court speaking through Utamwa, J considered an application in more or
less similar circumstances involving an elected member of parliament
whose membership in the sponsoring party was about to be terminated
which could have culminated into loss of his seat. Discussing the last
condition, Court said:
“….I agree …that the balance of
convenience is in favour of the Applicant in this matter for, in case
temporary injunction order is not issued, the feared irreparable loss
will become real, the main suit will become nugatory and thus the
Applicant will face more inconvenience than the Respondents and the
party generally will not suffer more inconvenience than the Applicant
because,... the order is not intended to restrain the Respondents from
their other functions generally….” (at page 45).
I am inclined to agree with my brother in his reasoning and that disposes the third condition in favour of the Applicants.
In the upshot, the application against the 1st, 2nd, and 3rd
Respondents [Board of Trustees - CUF, Lipumba na Magdalena Sakaya] is
hereby granted and the Court makes the following temporary orders of
Injunction as Follows:
1. Suspension of the implementation of
the expulsion Order issued against the Applicants from the Civic United
Front (CUF) Political Party pending the hearing and final determination
of Civil Case No. 143 of 2017 or any other order from the Court.
2. The 1st, 2nd and 3rd respondents, their agents, assignees or
anybody acting under their authority are restrained from in any shape or
form discussing the membership of the Applicants herein pending the
hearing and final determination of Civil Case 143 of 2017 or any other
order from the Court.
L. J. S. Mwandambo
JUDGE
Nakala ya Maamuzi haya tumeambatanisha na Taarifa hii
5. Ni kwa msingi huu Tarehe 20 Novemba, 2017 tulimuandikia Katibu wa
Bunge na ili amjulishe Mheshimiwa Spika Job Ndugai kuhusu Maamuzi haya
ya Mahakama Kuu ili naye achukue hatua stahiki ikiwemo kutufahamisha
utaratibu atakaoutumia kuturejesha katika nafasi zetu za Ubunge kama
ilivyokuwa awali ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
6. Tumeonelea ni vyema kuwajulisha wanaCUF na Watanzania kwa ujumla
hatua tulizozichukua baada ya Maamuzi ya Mahakama Kuu, na ni matarajio
yetu kuwa Mheshimiwa Spika na Mamlaka zake zote zitaheshimu Maamuzi ya
Mahakama Kuu.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa Leo Tarehe 27 Novemba 2017
Dar-es-Salaam.
………………………………………………….
RIZIKI SHAHARI MNGWALI
Kwa niaba ya:
1) MHE. SEVERINA SILVANUS MWIJAGE,
2) MHE. SAUMU HERI SAKALA,
3) MHE. SALMA MOHAMED MWASSA,
4) MHE. RAISA ABDALLAH MUSSA,
5) MHE. MIZA BAKARI HAJI,
6) MHE. KHADIJA SALUM ALLY AL-QASSMY, NA
7) MHE. HALIMA ALI MOHAMED,
Maoni
Chapisha Maoni