MBUNGE MSIGWA ALAUMU UKIMYA WA WASOMI NA KUMPONGEZA PROF MPANGALA WA CHUO KIKUU RUCU KWA KUWA MKWELI JUU YA TAIFA LAKE.
Iringa. Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ametoa lawama kwa wasomi nchini akidai wamekuwa wakikaa kimya hata pale wanapoona masuala ya Taifa hayaendi sawa.
Mchungaji
Msigwa amesema hayo wakati wa mjadala uliofanyika katika ukumbi wa Chuo
Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) wakati wa kongamano kujadili kitabu
kinachohusu miaka 70 ya kusaka demokrasia kwa nchi za ukanda wa Maziwa
Makuu kilichoandikwa na Profesa Gaudence Mpangala wa chuo hicho.
“Kwanza
nimpongeze Profesa Mpangala kwa kuja na utafiti huu ambao unaonyesha
hali ya kidemokrasia nchini bado iko chini, nchi hii inawategemea ninyi
wasomi ili iweze kusonga mbele, lakini kwa bahati mbaya mmetuachia sisi
vipofu ndio tunaowachaguliwa njia ya kupita,” amesema Mchungaji Msigwa.
Amesema,
“Upo usemi nimekuwa nikiutumia hata bungeni ‘akili ndogo kuongoza akili
kubwa’ na leo hapa niwaeleze kuwa licha ya kuwa Taifa linawategemea,
ninyi ndio mnaofanya tafiti bado mmeacha sisi wenye akili ndogo
kuwachagulia ngoma ya kucheza nanyi mnakubali kuicheza hata pale
mnapoona Taifa linatumbukia shimoni,” amesema.
Mchungaji
Msigwa amewataka wasomi kutimiza wajibu wao na kuwataka kutumia elimu
waliyonayo kushauri na kukosoa pale wanapoona inafaa kufanya hivyo.
Amesema
hatua hiyo itasaidia Taifa kujenga misingi bora ya demokrasia
inayoheshimu haki za binadamu na utawala bora na kusaidia kuinua uchumi
wa nchi.
Mwandishi
wa kitabu hicho, Profesa Mpangala amesema ili hali ya usawa wa
kidemokrasia nchini iweze kufikiwa ni lazima kuandika Katiba mpya kwa
kurejea maoni yaliyomo katika rasimu ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Maoni
Chapisha Maoni