Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Mambo ya kuzingatia ili uishi maisha marefu na yawezekana.
Kuishi ukiwa na afya na kuishi maisha marefu
kunawezekana kwa kubadili hali ya maisha unayoishi inayoharibu afya yako
mfano uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi,kutokufanya
mazoezi na kutokula matunda na mbogamboga.
Mambo yanayoweza kukusaidia kuishi maisha marefu ni kama yafuatayo
- Kuuandaa mwili kwa maisha marefu kwa kufanya mazoezi
- Kuwa makini kutambua na kutibu matatizo ya kiafya
- Kuepuka mazingira na kufanya kazi kwa namna au kazi zinazoweza
kudhuru maisha yako. Mfano kuendesha gari bila kufuata utaratibu,
kutokuvaa vifaa vya kujikinga wakati wa kazi
- Epuka vitu vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya yako na kukuletea
matatizo ya kiafya kama dawa za mimea na mifugo, zitumie kama
inavyotakiwa
- Usinywe pombe, usivute sigara wala kutumia dawa za kulevya
- Kula mlo kamili
- Usile vyakula vyenye chumvi na mafuta mengi
- Kunywa maji mengi ili kusafisha mwili
- Epuka msongo wa mawazo
Maoni
Chapisha Maoni