Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
PondÃ
ameachiwa jana Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu
jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano
wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."
Awali,
Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema uchunguzi dhidi ya
Ponda ulikuwa ukiendelea na kama ungekamilika angepewa dhamana.
"Upelelezi
unaendelea na ukikamilika tutaangalia kama atapata dhamana au
tutampeleka mahakamani," alisema Mambosasa kabla ya Sheikh Ponda
kuachiwa.
Wakili
wa Ponda, Profesa Abdallah Safari amesena: "Ni kweli Sheikh PondÃ
ameachiwa, ni lini atarudi tena sijajua ila sidhani kama watampeleka
mahakamani."
Maoni
Chapisha Maoni