Mara nyingi
wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile
yaawali wakati mnaanza mapenzi yenu.
Wanawake wengi wanalalamika kuwa
hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata
wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.
Mara zote hushuka
huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu
pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika,
muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo
zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata
tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana,
hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote
haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza
ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za kukusaidia
1. kucheka pamoja
Kicheko ni mlango
wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa
mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta
furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika
kila kitu. Jifunze kujizuia pale
unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.
Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine
kokote.
2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe
msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze
kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako
afanyavyo au apendavyo. Onyesha heshima katika
vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi
mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali
pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.
Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini
na kutunyanyua na sisi pia.
3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso
wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana
mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.
Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia
bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za
kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu
huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je,
ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?
Kugusana ndio
mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana
na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa
kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa
upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza
kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa
katika mahusiano yenu.
4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo
vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa
majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze
kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama vile
maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia
sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na
umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro
isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda
kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na
zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja
taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.
5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache
maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.
Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana,
na lazima tuwape
tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia
za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako
akuambie yanayo muumiza na msameheane.
6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi
hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia
unalindwa, pia muonekano wetu lazima ume
halisi na sio feki. Vile tunavyoviona
katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile
tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo
bora katika mahusiano yetu. Ukianza kupata ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako
utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake
utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe
kuvitafuta vile vyote mpenzi wako
alivyonavyo ambavyo hukuza ukaribu wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote
katika maisha yako.
Maoni
Chapisha Maoni