MITANDAO YA KIJAMII IMEKUWA NA MOTO MKALI KULIKO MIKUTANO YA KISIASA SASA SERIKALI YAHAHA ILA SHERIA ZIPO VIPI?
Naibu mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandaoni, Joshua Mwangasa amewataka
viongozi wa makundi ya whatsApp kutoa taarifa pindi uhalifu
unapofanyika katika makundi yao kwani kwa kiasi kikubwa makundi hayo
yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.
Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa kutapunguza na
kudhibiti makosa mengi yanayofanywa mtandaoni na kutasaidia polisi
kuchukua hatua dhidi ya muhusika aliyefanya uhalifu huo.
Lengo kubwa likiwi ni kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu
mtandaoni huku makundi ya What’s App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.
“Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka
mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata
wewe utahusika,” amesema Mwangasa.
Mwangasa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria
waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na
uhalifu.
“Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi
kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa
maendeleo,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema
mamlaka hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano
mtandaoni.
Hayo yamezungumwa jana katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es
Salaam.
Maoni
Chapisha Maoni