Mwanasoka wa zamani George Weah anaongoza kwa kura pia Wanasoka mbalimbali duniani wajipanga kufata nyao za Weah.


Mwanasoka wa zamani George Opong Weah anaongoza, katika matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Liberia.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzio NEC zinaonyesha Weah yupo mbele kwa majimbo 11 katia ya majimbo 15 japo kura zote hazijahesabiwa.
Mgombea anayefuatia ni makamu wa rais Joseph Boakai,ambaye anaongoza katika jimbo moja na mengine yanayosalia ameshika nafasi ya pili.
Mshindi katika kinyang'anyiro hicho analazimika kujipatia asilimi 50 ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi,na kama hakuna mgombea atakayefikisha kiwango hicho,uchaguzi wa marudio unapaswa kuwa mwezi Novemba.

Atakayetangazwa mshindi anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel.







Maoni