Mamlaka
ya Hali ya Hewa (TMA), imewatahadharisha wadau, wanajamii na sekta
zinazojishughulisha na mazingira juu ya mafuriko yanayoweza kutokea
katika kipindi cha mvua za msimu zinazotarajiwa kuanza kunyesha kati ya
mwezi Novemba na Aprili 2018.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agnes Kijazi ameeleza hayo leo
Jumanne, Oktoba 17, na kusema kuwa katika kiipindi hicho kunatarajiwa
kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo mbalimbali nchini
ambavyo vinaweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo.
Dkt.
Kijazi amewataka wadau wa sekta mbalimbali zinazohusiana na mazingira
kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa ili
kuondokana na madhara yanayoweza kuepukika.
“Wadau wa sekta ya uvuvi, kilimo, mifugo, chakula na wanyamapori wanatakiwa kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya hewa. Kufahamu mapema kutasaidia kujipanga,” alisema Dkt. Kijazi.
Aliongeza
kuwa kufuatia mvua hizo zinazotarajiwa, kiwango cha unyevu katika
udongo kitaongezeka na hivyo kuwataka wachimbaji wa wadogo wa madini
kuchukua tahadhari kwani unyevu huo unaweza kupelekea mmomonyoko wa
ardhi na kuleta maafa.
Aidha,
amezitaka mamlaka za miji na sekta mbalimbali kuhakikisha wanafanya
ukaguzi wa mitaro na mifereji ya kupitisha maji iwe inafanya kazi muda
wote ili kuepusha kutuama kwa maji na kusababisha mafuriko pamoja na
maonjwa ya milipuko.
“Sekta ya afya ichukue hatua stahiki ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyoweza kusababisha milipuko ya magonjwa,” amesema Dk Kijazi.
Maoni
Chapisha Maoni