Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema linatarajia
kutoa msimamo wao hivi karibuni kufuatia kauli ya Rais Magufuli ya
kutoongeza mshahara, mara baada ya vikao vyao na serikali kufanyika.
Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa amesema wanakusudia kuonana na
uongozi wa serikali ili kujadili suala hilo, na ndipo watatoa msimamo
wao kama hawatafikia makubaliano mazuri.
“Tunahitaji kuonana na uongozi wa serikali tujadili, kuna mambo mengi ya
kujadili sio la mishahara tu, kwa muda mrefu vikao vimekuwa havikaliwi,
hata vikikaliwa havina majibu, sasa hivi lazima tulitafutie ufumbuzi
kwa sababu changamoto ni nyingi, wafanyakazi hawana hali nzuri kabisa,
malalamiko ni mengi mno”, amesema Yahya Msigwa.
Maoni
Chapisha Maoni