Ruka hadi kwenye maudhui makuu
BODI YA MKOPO YATOA ORODHA MPYA, WANUFAIKA WA MIKIPO YA ELIMU YA JUU
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha
nyingine kwa wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata
mikopo.
Hivyo idadi hiyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza
waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353. Katika Awamu ya Kwanza,
wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili
(11,481), Awamu ya Tatu (7,901).
Tumekua tukifanyia kazi orodha za udahili ambazo tumekuwa tukipokea,
na kila tunapokamilisha, tunatoa orodha za wanafunzi waliopangiwa
mikopo ambao wana sifa – leo tumetoa hao 1,775”, amesema Mkurugenzi
Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru
Badru, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari pia amekumbusha kuwa
kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya
wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi
147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.
Maoni
Chapisha Maoni