Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka
miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa
anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.
Hukumu
hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi
hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila
kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo
cha miaka miwili jela.
Ushahidi
wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani
mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya
mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, kwa mujibu wa
mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehemu, marehemu alilewa lakini
kuhusu mshtakiwa anatakiwa kutoa maelezo yanayo jitosheleza, kwa hili
mshtakiwa alijikanganya" amesema Jaji Rumanyika.
Jaji
Rumanyika ameendelea kwa kusema kwamba.."mshtakiwa katika maelezo yake
hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, maelezo ya
Dkt. Josephine siyo maelezo ya cheti cha hospitali, hayakuwa na hadhi
ya hospitali".
Inakinzana
na hekima ya kawaida kwamba hata pale marehemu alipoendelea kumpiga na
kumshambulia na akaenda kiwango cha kumtishia kumuua, mshitakiwa
hakuthubutu hata kumpiga, ina maana alifanya kama maneno ya biblia
yanavyosema mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia lakini
hili mshitakiwa hakulisema.", amesema Jaji Rumanyika.
Na
wakati huo mshitakiwa alikuwa na miaka 17, leo ana miaka 22, alikuwa
mtoto hivyo asingetambua kuwa kinachofanyika ni kibaya au kizuri, huyu
mtoto sio mshtakiwa aliyelengwa na sheria ya watoto, kama mtoto wa umri
huu na anaweza kafanya ya watu wazima, mahakama hii haikubaliani bali
mshtakiwa ni mkomavu, hakuna mashaka kuwa kifo cha marehemu kilitokana
na ugomvi", ameendelea kusema Jaji Rumanyika mahakamani hapo.
Baada
ya hapo jaji rumanyika aliwapa nafasi upande wa mshtakiwa kujitetea
ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshitakiwa kwa kusema kuwa
mshitakiwa anategemewa na familia yake.
Baada ya hapo Jaji Rumanyika alitoa hukumu yake na kumuamuru mshitakiwa kwenda jela kwa miaka miwili.
Elizabeth
Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa mpenzi wake Steven
Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, mnamo April 7, 2012.
Maoni
Chapisha Maoni