ITALY IMESHINDWA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018.

 

Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italy wameshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi ikiwa ni mara yao ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden.

Hii ina maana kuwa Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa kwake kwa mara ya kwanza mwaka 1930 ambapo timu iliilishiriki.

Aidha, kwa upande wake kiungo, Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.

Katika mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua, wengi walitarajia kuwa Italia ingeweza kushinda kwa ilikuwa ikiutumia uwanja wa nyumbani wa San Siro huku historia ikiwapa nafasi kubwa timu hiyo ya Azzuri.

Hata hivyo, Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 langoni mwa timu ya Sweeden lakini bahati haikuwa upande wao, kwani pamoja na mashuti hayo hawakuweza kupata hata bao moja.

 Matokeo hayo yanaifanya Sweden kushiriki mashindano hayo tena tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.

Maoni