Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Jeshi la Zimbabwe latoa sababu kuweka vifaru mitaani na Urais wa Mugabe
Jeshi la Zimbabwe limetumia kituo cha habari cha Taifa (ZBC) kueleza
lengo la kuingiza mitaani silaha nzito za kivita ikiwa ni pamoja na
vifaru.
Jeshi hilo ambalo lilichukua hatua hiyo saa chache baada ya kuviambia
vyombo vya habari kuwa halitasita kuingilia kati mgogoro wa madaraka
ndani ya chama tawala cha Zanu-PF baada ya Rais Mugabe kumfukuza
aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa limesema hatua hiyo
imelenga kuwasaka wahalifu na sio vinginevyo.
Kupitia tamko lake kwa vyombo vya habari, jeshi hilo limesisitiza
kuwa hakukuwa na mpango wa kufanya mapinduzi ya kijeshi na kwamba Rais
Mugabe na familia yake wako salama na walikuwa wanajua kinachoendelea.
Hata hivyo, hawakuainisha ni walafu gani waliokuwa wanasakwa ndani ya nchi hiyo na silaha nzito za kivita.
Tungependa kulihakikishia taifa kuwa mheshimiwa Rais na familia yake
wako salama na ulinzi wao ni wa uhakika,” limeeleza tamko lililosomwa
na Meja Generali, Gen Sibusiso Moyo.
Tunalenga wahalifu wanaomzunguka ambao wanapanga matendo ya
kihalifu, ambao wanasababisha mateso ya kijamii na kiuchuni nchini.
Punde tutakapokamilisha mkakati wetu, hali ya kawaida itarejea,”
aliongeza.
Kutokana na vitendo hivyo vya jeshi, Balozi za Marekani na Uingereza
zilitoa tamko kwa raia wake waliopo nchini humo, zikiwataka kutotoka nje
ya nyumba zao hadi hadi hali itakaporejea kwenye ukawaida.
Rais Mugabe alimfuta kazi Mnangagwa kwa madai kuwa anapanga njama za
kumhujumu na kutaka kumrithi bila kufuata taratibu za kichama. Alisema
Mnangagwa amekuwa akienda kwa waganga na watabiri akitaka kujua Mugabe
atakufa lini.
Kutokana na hatua hiyo ya Mugabe, Mkewe mama Grace anatajwa kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kurithi nafasi ya mumewe.
Maoni
Chapisha Maoni