Ruka hadi kwenye maudhui makuu
KUTOKA DODOMA BUNGENI WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA KUHUKUMIWA JELA MAISHA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amewasilisha muswada
Bungeni na kusema kuwa atakayetiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha
mirungi au bangi zaidi la kilo 50 atahukumiwa kifungo cha maisha
gerezani.
Mapendekezo hayo ni kwa lengo la kudhibiti ongezeko la
wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya , kupunguza uuzaji na
usambazaji dawa za kulevya.
Adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, kwa mujibu wa muswada huo, ni
kwa wanaowaweka rehani watu ili kufanikisha biashara ya dawa za kulevya,
wamiliki wa mitambo ya kutengeneza dawa hizo na watakaowaingiza watoto
kwenye matumizi na biashara ya dawa za kulevya
Amesema masuala ya msingi yaliyozingatiwa kwenye muswada huo ni
kuharamisha baadhi ya vitendo, kuweka adhabu, kuidhinisha vigezo vya
kufuata wakati wa utoaji dhamana na uwezo wa mahakama katika kusikiliza
mashauri yanayotokana na sheria hiyo.
Mhagama amesema kifungu cha 15(1) cha muswada huo kimependekezwa
kuongezwa kipengele (C) ili kuweka katazo la kuwezesha au kusababisha
mtu kusafirishwa nje ya nchi kuwekwa rehani ili kufanikisha biashara ya
dawa za kulevya.
“Kipengele hiki kinaweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu
atakayekiuka masharti ya kifungu hicho. Vilevile kifungu kidogo cha pili
kimerekebishwa kwa kuzuia yeyote kujihusisha isivyo halali na kemikali
zinazotumika kutengenezea dawa za kulevya.
Aidha amesema kuwa Kifungu cha 29, kimefanyiwa marekebisho kwa malengo ya kuongeza makosa yasiyostahili dhamana.
Maoni
Chapisha Maoni