Aidha, kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Atashasta Nditiye alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema
kuwa hawezi kulizungumzia kwa sababu waziri mkuu yupo na wao hawajapata
taarifa yeyote.
Naomba utambue kuwa katibu mkuu bado yupo Canada kwa hiyo mambo
mengine mimi siyafahamu hadi atakaporudi atujulishe kilichojiri huko
Canada,”amesema Nditiye
Akizindua uwanja wa ndege wa mjini Bukoba, Novemba 6, mwaka huu, Rais
Dkt. Magufuli alisema kuwa amemuandikia barua waziri mkuu wa Canada
kumuomba kuachiwa kwa ndege hiyo na akaongeza kuwa amemtuma mwanasheria
mkuu wa serikali, George Masaju kushughulikia suala hilo.
Hata hivyo, ndege hiyo ya Bombardier Q400-8 inashikiliwa kwa amri ya
mahakama nchini humo kutokana na shauri lililopo kati ya serikali na
kampuni ya Stirling Civil Engineering.
Maoni
Chapisha Maoni