Ruka hadi kwenye maudhui makuu
MAREKANI YAITAKA DUNIA KUSITISHA BIASHARA NA KOREA YA KASKAZINI.
Marekani imetoa wito kwa mataifa
mbalimbai kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na kibiashara na Korea
Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kupinga majaribio ya makombora ambayo
yamekuwa yakifanywa na taifa hilo.
Balozi wa Marekani Nikki Haley,
ametoa pendekezo hilo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la
umoja wa mataifa unaoendelea mjini New York.
Bi. Haley amesema
kuwa Rais wa Marekani amemtaka Rais wa China Xi Jinping kusitisha
biashara ya mafuta ghafi na Korea Kaskazini, kama sehemu ya kutekeleza
hatua ya kuwekewa vikwazo kwa taifa hilo.
Kupitia hatua hii ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini tunapaswa
kusitisha asilimia tisini ya biashara na Korea Kaskazini pamoja na
asilimia 30 yamafuta yake.
Msambazaji mkubwa wa mafuta Korea Kaskazini ni China.
Mwaka 2003, China ilisitisha kupelekea mafuta Korea Kaskazini ,muda
mfupi baadaye taifa hilo likasogea katika meza ya majadiliano.
''Tumefikia
hatua ya kuitaka China kuchukua hatua Zaidi katika hili, ni lazima
isitishe kuipatia mafuta Korea Kaskazini," alisema Haley.
Wajumbe
wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wanakutana mjini Ne York
kujadili hatua ya Korea kaskazini na majaribio ya makombora ya masafa
marefu.
Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa Stéphane Dujarric,
amesema kuwa Antonio Guterres, amelaani hatua hiyo Korea Kaskazini na
kuongeza kuwa huo ni ukiukaji wa maamuzi ya baraza la usalama la umoja
wa mataifa.
Source Bbc
Maoni
Chapisha Maoni