MATAMKO YA MAWAZIRI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAENDELEA KUWATOKEA PUANI WENYEWE KWA KUKURUPUKA NA MATAMKO.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii
Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo
Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na
Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa.
Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh.
Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na
kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu.
Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla
alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja
mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu
nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea,"
Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri
Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba
Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao
"Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu sana.
Tuongee kindugu nje ya hapa! Kuweka sawa ni kwamba 'sikukutaja!"
Kigwangalla.
Hivi karibuni Waziri Kigwangalla aliweka wazi kwamba amewaondoa Askari
wote wa kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na
mwekezaji huyo ambaye ana uhusiano wa Karibu na Prof. Songorwa
(aliyemsimamisha kazi siku chache zilizopita) na alikuwa na uhusiano ya
karibu na Prof. Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri
wa Maliasili na Utalii wa zamani.
Balozi Kagasheki aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika
uongozi wa serikali ya awamu ya nne ambapo aliongoza wizara hiyo Mwaka
(2012-2013)
Maoni
Chapisha Maoni