Ruka hadi kwenye maudhui makuu
MBUNGE WA KIBAMBA MNYIKA ASEMESEMA BOMOABOMOA YA KIMARA ILIKUWA HARAMU
Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika amesema kuwa
bomoabomoa iliyofanyika Kimara jijini Dar es salaam, ni haramu kwasababu
sheria iliyotumika ilitungwa mwaka 1932 na ilishafutwa.
Amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli katika ziara yake ya Mwanza alitoa
kauli ya kibaguzi na kama si ya kibaguzi basi serikali itoe kauli ya
kuwalipa fidia wakazi hao waliobomolewa nyumba zao.
“Kwasababu Serikali ilisingizia sheria lakini mimi kama mbunge
nilichukua hatua ya kuleta marekebisho ya sheria bungeni ili barabara
yote iwe mita 60, lakini serikali ikafanya njama na katibu wa bunge
(Thomas Kashilillah) kuzuia huo mswaada,”amesema Mnyika
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Elias
Kuandikwa amesema kuwa sheria mbalimbali za barabara zilipokuwa
zikitungwa zilikuwa zinazingatia maendeleo hivyo sheria ya mwaka 1932
iliainisha ukubwa wa barabara popote ilipokuwa inajengwa.
Hata hivyo, Kwandikwa amemtaka mbunge huyo kuwasiliana na mamlaka ya
halmashauri za serikali za mitaa ambao ndio wasimamizi kuona kama kuna
mahitaji kwa baadhi ya maeneo kufanyiwa marekebisho ya sheria
Maoni
Chapisha Maoni