Ruka hadi kwenye maudhui makuu
MGAO WA UMEME KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI TANZANIA WAMFANYA NAIBU WAZIRI WA NISHATI KUTOA NENO
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa Tanesco
kuhakikisha kuwa hawakati umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea
wananchi adha ya kukosa huduma hiyo.
Subira ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa
TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za
Umeme vya Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.
Amesema kuwa umeme ukatike pale inapostahili tu na endapo tatizo
linatokea kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu Tanesco ikatoa taarifa mapema
kwa wananchi,na kwamba kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli
nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato wananchi.
Aidha, Naibu Waziri amewaagiza watendaji wa Tanesco wanaosimamia
mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo
inakamilika tarehe 15 Desemba mwaka huu.
Hata hivyo, Mradi wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo
Vipya 19 vya kupoza Umeme wa Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na
ujenzi wa njia za Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika
Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Kilimanjaro na utagharimu Dola milioni
43 zilizotolewa na Benki ya Dunia.
Maoni
Chapisha Maoni