Ruka hadi kwenye maudhui makuu
RAIS MUGABE AGOMA KUN'GOKA MADARAKANI
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amesema kuwa yeye bado ni kiongozi
halali wa nchi hiyo na kukataa upatanishi unaofanywa na Kasisi mmoja wa
Kanisa Katoliki ili kuwezesha mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani
baada ya jeshi kuchukua udhibiti tangu siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini humo, Kasisi Fidelis Mukonori,
amejitolea kuwa mpatanishi kati ya Majenerali wa Jeshi na Rais Mugabe,
ingawa hakuna taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo yenye lengo la
kuepusha umwagaji damu baada ya Mugabe kuondoka madarakani.
Aidha, taarifa zaidi zimesema kuwa Makamu wa Rais aliyetimuliwa,
Emmerson Mnangagwa, amekuwa akiandaa mpango wa uongozi baada ya Mugabe
kuondoka madarakani akishirikiana na jeshi pamoja na upinzani kwa zaidi
ya mwaka mmoja sasa.
Hata hivyo, kiongozi wa chama cha upinzani nchini humo cha MDC,
Morgan, Tsvangirai, ambaye amekuwa akipatiwa matibabu ya Saratani nchini
Afrika Kusini na Uingereza amerejea Zimbabwe na kumtaka Rais Mugabe
kung’atuka kwa amedai kuwa ameishiwa uwezo wa kuiongoza nchi hiyo
Maoni
Chapisha Maoni