Ruka hadi kwenye maudhui makuu
UKUWAJI WA UCHUMI NCHINI TANZANIA UPO VIZURI KAULI YA WAZIRI MKUU ILA WANANCHI WANAHOJI MBONA HALI YA NCHI NI MBAYA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa amesema mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Taifa
unaridhisha, ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa
asilimia 5.7.
Majaliwa amesema hayo wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Bunge, mjini Dodoma Novemba 17, 2017.
Mwenendo wa uchumi wetu ni wa kuridhisha,
mfano, ukuaji wa uchumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa
asilimia 5.7, robo ya pili ilikuwa asilimia 7.8 na nusu ya kwanza ya
mwaka huu ilikuwa ni asilimia 6.8.”
Majaliwa amesema hali hiyo inafuatia
kuongezeka kwa makusanyo ya kodi na usimamizi thabiti wa matumizi ya
Serikali, ambapo nakisi ya bajeti ya Serikali imeshuka na kufikia
asilimia 1.9 kwa mwaka 2016/2017
Pia amesema akiba ya fedha za kigeni
inatosheleza kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa zaidi ya kipindi
cha miezi mitano, ikiwa ni zaidi ya lengo la miezi minne.
Akizungumzia kuhusu kasi ya upandaji bei,
Waziri Mkuu amesema takwimu zinaonyesha kwamba katika nusu ya mwaka
2017, mfumuko wa bei uliendelea kubaki katika kiwango cha tarakimu moja.
“Takwimu zinaonyesha kwamba mfumuko wa bei
nchini kwa mwezi Oktoba 2017 ulikuwa ni asilimia 5.1 ikilinganishwa na
asilima 5.3 mwezi Septemba, 2017.”
Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei
kumechangiwa na kupungua kwa bei wa bidhaa za vyakula, ambavyo
vimepungua kutoka wastani wa asilimia 9.3 mwezi Septemba, 2017 hadi
asilimia 8.8 mwezi Oktoba, 2017.
Maoni
Chapisha Maoni