Ruka hadi kwenye maudhui makuu
WAZIMBABWE WASHEREKEA USIKU KUCHA JUU YA KUTOKA KWA DICTATOR MUGABE.
Shangwe na nderemo vilitawala katika mji mkuu wa Zimbabwe,
Harare na kwingineko nchini humo mara tu baada ya Spika wa Bunge, Jacob
Mudenda kuisoma barua ya Rais Robert Mugabe kujiuzulu wadhifa wa rais
kwa hiari yake.
Tangazo hilo la kushtukiza lilisomwa katika kikao maalumu cha bunge
na seneti, ambacho kilikuwa kimeanza mchakato wa kisheria ambao hatimaye
ungemng’oa Mugabe madarakani,
Aidha, Mugabe alisema katika barua yake ya kujiuzulu kuwa amefanya
hivyo kwa kuzingatia maslahi ya taifa, na kuwapa nafasi watu wengine ili
waweze kuiongoza nchi hiyo katika nyanja tofauti tofauti.
Rais Mugabe alimfukuza kazi makamu wake wa Rais, Emmarson Mnangagwa
wiki mbili zilizopita, hatua ambayo ilichukuliwa na wanaharakati
mbalimbali kama kumtengenezea njia mkewe Grace kuwa mrithi wa kiti cha
urais.
Hata hivyo, Jeshi la nchi hiyo limehimiza utulivu na kuheshimu sheria
wakati wa shamra shamra zinazoendelea, huku Kamanda Mkuu, Constantino
Chiwenga amesema kuwa vitendo vyovyote vya fujo na ulipaji kisasi
vitakabiliana na mkono mkali wa vyombo vya usalama.
Maoni
Chapisha Maoni